Kigogo adakwa kwa tuhuma za kughushi

Rai - - MBELE -

“Kwa hiyo mimi, Afande Mambosasa au kamanda yeyote wa kanda hatuwezi kulizungumzia hilo, mtafute msemaji wa jeshi, Barnabas Mwakalukwa ndiye anaweza kuwa na ufafanuzi au kulizungumzia hilo,” alisema Kamanda Abdul.

Msemaji wa Jeshi la polisi, Mwakalukwa alipoulizwa kupitia simu yake ya kiganjani alisema anayeweza kulizungumzia suala hilo ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai.

“Kama alikuwa Selander basi wasiliana na DCI, na kama anaripoti Kamata wasiliana na huyo huyo au msaidizi wake, maana kama liko chini ya upelelezi wa makosa ya jinai, hayuko chini ya Kamanda wa Kanda Maalumu au Kamanda wa Polisi Ilala.

“Hilo moja kwa moja liko ngazi ya kitaifa kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai au Kamishna wa Upelelezi, yeye ndiye anajua na ndiye atakupa taarifa. Hawa wengine hata kama litakuwa chini ya himaya yao, lakini kwa maelekezo ya DCI ndiye anayeweza kukupa taarifa unazotaka hawa wengine hawawezi kuliongela hilo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.