Kwa nini minada haifanikiwi?

Rai - - MAKALA - Ole Mushi 0712702602.

Hii ni mara ya pili mnada unaendeshwa hapa nchini na mambo hayaendi kama yalivyopangwa. Hali ni tofauti na zamani kidogo, mimi sio mtaalamu wa masuala ya uchumi ila minada hii inatoa viashiria vya hali halisi ya uchumi tulionao kwa sasa

Toka Serikali ya awamu ya tano ianze operation suala la ubanaji wa fedha umekuwa ukitiliwa mkazo sana. Mojawapo ya njia inayotumika ni Serikali kutokufanya biashara na sekta binafsi.

Mfano mikutano iliyokuwa ikifanyika kwenye kumbi za hoteli binafsi sasa hivi zinafanyikia kwenye kumbi za majengo ya Serikali. Tumeshuhudia mahoteli yakifungwa muda mfupi ujao shule binafsi pamoja na vyuo binafsi navyo vitaanza kuzorota na kufungwa.

Kwangu mimi binafsi naona kuna faida ila pia kuna hasara zake. Faida za kubana sana fedha ni kufanya bidhaa kushuka bei. Yaani watu wanapokuwa hawana fedha mfukoni bei ya vitu hushuka kwa mfano kiwanja ulichouziwa kwa shilingi milioni 50 mwaka 2014 leo huwezi kukiuza kwa bei hiyo lazma ukishushe bei kwa kuwa watu hawana fedha. Au hotel ambayo ulikuwa ukilala kwa Dola za Marekani 100 sasa hivi unaweza kulala kwa Dola za Marekani 50.

Faida ya pili ni kwamba kwa kuwa watu hawana fedha basi watalazimika kuzitafuta. Tafsiri yake ni kuwa utendaji kazi utaongezeka, watu wameongeza bidii katika kutafuta fedha watu hawalali ukilala basi ukubali kulala njaa tija.

Pamoja na faida hizo ila Ubanaji wa fedha sana unahasara zake. Hasara moja kubwa ni kwamba biashara zinakufa au Uzalishaji unakufa. Yaani kutokana na gharama za Uzalishaji kutokuendana na bei Iliyopo sokoni lazma wazalishaji wapate hasara. Tunaona baadhi ya biashara zikifa au kufungwa hii ni kutokana na kuwa watu hawana fedha za kununua na ndio kinachotokea kwenye minada inayoendeshwa nchini.

Kutokana na biashara au zalishaji kufa basi wigo wa watu kupata ajira unapungua. Kwa mfano ukifunga kiwanda au hotel basi waliokuwa wanafanya kazi hapo wanarudi nyumbani.

Hasaraa nyingine ni kuwa watu wanafanya Savings za fedha zaidi kuliko kuzitumia. Watu hawana uhakika wa kesho hivyo wanajitahidi Kusevu. Hii inapunguza mzunguko wa fedha mtaani. Watu wanapokosa pesa biashara zinakuwa hazifanyiki, watu wanapunguzwa makazini au kushushwa mishahara.

Kwa maana hiyo Dk. Shika alijua ule mchezo aliokuwa anacheza hakuna wa kufika mwisho maana watu hawana fedha ..... upepo ni ule ule unaonekana hapa kwenye Makontena.

Kupanga ni kuchagua aidha tuzibane zaidi au tuziachie...

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.