Nyota ya Taifa Stars iko Uganda

Rai - - MAKALA JAMSEPITIEMBA - NA MWANDISHI WETU

WIKI nyingine muhimu kwa timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ imewadia. Ni wiki ambayo mataifa kadhaa yatakuwa yakipambana kuwania kufuzu kwa fainali zijazo za Afcon huku Tanzania ikiwa ni mojawapo.

Taifa Stars itakuwa ugenini Jumamosi ijayo kucheza na Uganda ‘The Cranes’ katika uwanja wa Mandela, Namboole jijini Kampala kutafuta pointi muhimu zitakazowafanya kuvuka hatua hiyo ya makundi.

Taifa Stars iko kundi L pamoja na Uganda, Lesotho na Cape verde huku ikiaminika ni moja kati ya makundi mepesi sana ukilinganisha na mengine katika michuano hiyo .

Awali Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) lilipotangaza makundi pamoja na ratiba ya mashindano hayo wadau wengi wa soka hapa nchini waliamini kuwa Tanzania imepangwa kundi rahisi kwavile haikuwa pamoja na timu za mataifa ya magharibi au kaskazini mwa Afrika.

Hata hivyo katika soka hakuna timu ya kubeza kwani kadiri siku zinavyosonga mbele ndivyo mataifa mengi yamekuwa na mageuzi makubwa katika mchezo huo hivyo dhana hiyo kukosa mashiko.

Mpaka sasa Taifa Stars imeshacheza mchezo mmoja wa kundi hilo dhidi ya Lesotho Juni mwaka jana hapa jijini Dar es salaam na kutoka sare ya bao 1-1. Mchezo unaofuata ni dhidi ya The Cranes utakaofanyika jijini Kampala, Uganda mwishoni mwa wiki hii matokeo kwa Taifa Stars ni muhimu kuliko kitu chochote kile kwa sasa.

Matokeo yatarudisha imani kubwa iliyopittea kwa mashabiki wengi kiasi cha kutoipa sapoti kubwa timu hiyo na badala yake kuzigeukia timu za vijana kama vile Serengeti Boys na Ngorongoro Worriers.

Ni mchezo muhimu kwa Taifa Stars kutokana na ukweli kuwa Uganda ndiyo timu ngumu na pinzani zaidi kwa Taifa Stars ukilinganisha na Lesotho na Cape Verde.

Kihistoria Uganda imekuwa ikiongoza katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki na hata zinapokutana timu za taifa rekodi zinaonyesha The Cranes kuinyanyasa zaidi Taifa Stars.

Matokeo kwa taifa Stars katika mchezo huo ni dhahiri itakuwa kujisafishia njia kuelekea fainali hizo zinazotarajiwa kufanyika mwakani nchini Cameroon.

Mpaka sasa Uganda ina pointi tatu baada ya kushinda mchezo wake wa kwanza dhidi ya Cape Verde Juni 11 mwaka jana ikiwa ugenini. Taifa Stars inafungana na Lesotho kila moja ikiwa na pointi moja hivyo kuwa nyuma ya Uganda huku Cape Verde ikiwa mkiani mwa kundi hilo bila ya pointi.

Taifa Stars ili ifuzu fainali hizo inawapaswa kuzichanga vema karata zake katika mchezo dhidi ya Uganda kwani ikiifunga ni wazi inajirahisishia njia kwakuwa ndiyo timu ngumu katika kundi hilo.

Hiyo haimaanishi kuwa Cape Verde na Lesotho ni timu za kudharauliwa hapana isipokuwa ubora wao ni tofauti kubwa sana na waganda ambao kwa mujibu wa rekodi za FIFA ndiyo wanaoongoza katika ukanda huu kwa kusimama katika nafasi ya 83 ulimwenguni wakifuatiwa na Kenya (105), Tanzania (121), Rwanda (125) na Burundi (136).

Kwa upande wa michuano ya kuwania kufuzu afcon ijayo kutoka kundi L Uganda iko juu ikifuatiwa na Caep Verde (106) ikifuatiwa na Tanzania na mwisho Lesotho (147).

Lakini ukiangalia kw aupande wa Afrika i wazi kila timu imedhamiria kufanya maajabu katika kundi L ili kufuzu hivyo haitashangaza kuona Lesotho

ama Cape zikiibuka nafasi za juu kinachotakiwa ni maandalizi na umakini katika kuzicheza mechi zao.

Tanzania imedhamiria kushinda mechi hiyo ili kujikusanyia mtaji na katika kuthibitisha hilo mbali na kuitwa nyota wake wanaocheza nje pia imeleta kocha mpya kutoka Nigeria, Emmanuel Amunike kuinoa Taifa Stars.

Amunike tayari ameweka wazi kuhitaji pointi zote 15 katika mechi zote tano zilizosalia ili kujihakikishia anaweka rekodi na kuipeleka Stars katika fainali hizo kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo miaka 38 iliyopita.

Amunike amewaita nyota wote wa Tanzania wanaocheza nje akiwemo nahodha wake Mbwana Samatta anayecheza nchini Ubelgiji, Thomas Ulimwengu (Sudan), Himid Mao (Misri ), Abdi Banda (Afrika Kusini), Shaban Chilunda (Hispania), na Simon Msuva (Morocco).

Hofu kubwa waliyonayo baadhi ya wadau nchini ni kutokana na kuitwa kwa baadhi ya wachezaji wa kikosi cha pili baada ya wale wa kwanza kusimamishwa na TFF kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Wachezaji waliosimamishwa lakini baadaye kutolewa ahadi ya kujumuishwa wakati mwingine ni Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Jonas Mkude, Shiza Kichuya na John Bocco kwa upande wa Simba pamoja na Feisal Salum wa Yanga. Walioitwa kuziba nafasi zao ni Salum Kimenya, Frank Domayo, Ali Sonso, David Mwantika, Salum Kihimbwa, Kelvin Sabato na Paulo Ngalema.

Kwa upande wa Uganda ni kama imedhamiria zaidi kwani imeitwa karibu kikosi kizima kutoka nje kuja kuivaa Taifa Stars.

Katika orodha hiyo wapo nyota wanaofanya vizuri barani Ulaya wakiwemo……

Vyovyote itakavyokuwa taifa stars wanatakiwa kuipa umuhimu mechi hiyo kwakuwa ndiyo itakayoweza ama kuwajenga zaidi kisaikolijia iwapo watashinda la watapoteza basi watakuwa na kazi kubwa baadaye ya kujirudisha katika mstari kifikra achilia mbali ile kazi ya kushinda mechi zinazofuatia katika mwezi Oktoba na Novemba ili kurejesha imani.

Kitu pekee kitakachoisaidia ni maandalizi mazuri ukiwemo mshikamano miongoni mwa kikosi wenye kwa wenyewe lakini pia miongoni mwa mashabiki na wadau wengine ukiwemo uzalendo kwa watanzania wote kama taifa.

Ikumbukwe mshindi wa kwanza kutoka kila kundi nyte atakayefuzu kucheza fainali lakini pia timu zingine tatu kutoka makundi tofauti zitakazomaliza nafasi ya pili zikiwa na wastani mzuri zaidi (washindi bora) zitapenya kucheza fainali hizo mwakani.

Watanzania wanaamini matokeo mazuri kule Uganda italeta nuru kwao katika safari mpya ya Taifa Stars kuelekea fainali zijazo za Afcon hapo mwakani nchini Cameroon.

Kikosi cha Taifa Stars

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.