NUNUA KURA, MCHEZO MPYA AFRIKA

Rai - - MBELE - NA BALINAGWE MWAMBUNGU

NIGERIA imekuwa miongoni mwa nchi za Kiafrika zinazopigiwa chapuo kwamba imeweza kuendesha chaguzi mbali mbali na kubadili uongozi wa juu wa nchi bula mamatizo. Lakini uchaguzi mkuu ujao, huenda ukabadili sura hiyo kutokana na taarifa kwamba kuna mchezo wa kukunua kura na wanasiasa kuhama vyama vyao kwa sababu hawaridhiki na tawala zilizopo.

Lakini Tanzania imetia fora katika kipindi cha miaka mitatu tangu ufanyike Uchaguzi Mkuu 2015, imeshuhudia vituko ambavyo havikuwahi kutokea huko nyuma— Madiwani na Wabunge kujivua uwanachama na kujiunga na chama kilicho madarakani, kwa sababu za kipuuzi tu—eti wanamwunga mkono Rais John Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya.

Nasema ni sababu za kipuuzi kwa sababu Rais anatakiwa afanye kazi yake vizuri ili kutekeleza malengo na ilani ya chama chake. Alikuwapo Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) wakati huo, aliwalalamikia wandishi wa habari kwamba walikuwa waliandama shirika kwa kuandika mabaya tu. Akadai mbona mazuri hamwandiki? Akajibiwa kwamba mambo yakienda vizuri, ndio wajibu wa viongozi—wanafanya kazi vizuri, ndio matarajio ya wadau— kwamba mwendeshe shirika vizuri!

Vyama vya upinzani ni kama wandishi wa habari, ndio jicho la wananchi—kuona kwamba kiongozi wa juu na wasaidizi wake, wanafanyakazi zao vizuri. Upinzani ukiwa dhaifu na ukadhoofishwa— kama hivi wanavyofanya Madiwani na Wabunge wa upinzani, wanadhoofisha ufanisi wa Serikali kufanya kazi yake vizuri—itimize wajibu wake.

Tanzania kuna madai ya viongozi kununuliwa. Kule nchini Nigeria mambo kidogo ni tofauti— vinanunua wapiga kura wakati wa chaguzi. Vinaweka mawakala wa kununua kura kutoka kwa wananchi wazi wazi, kiasi kwamba tayari kuna hofu kwamba uchguzi mkuu ujao, hautakuwa huru na wa haki. Kwamba inawezekana chama chenye hela nyingi ndicho kitakacho nyakua ushindi.

Lakini kuna jambo jingine kubwa huenda likatokea Nigeria— Magavana wa Majimbo sita k M P w t a t w k

k a o w t s z k w k S

k k l z k k a

v s n K il

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.