Mitandao ya kijamii na jitihada za kusimamia ‘mabaya’

Rai - - KIMATAIFA / KATUNI - NA HILAL K SUED

KILA siku ya Jumanne makao makuu ya mtandao wa Facebook na kila Ijumaa makao makuu ya mtandao wa YouTube, watendaji wakuu hukutana kujadili changamoto mbali mbali zinazojitokeza kuhusiana na jumbe za chuki,

habari za uongo na jumbe nyingine zisizofaa katika mitandao yao, na kuamua kipi kiondolewe na kipi kibakizwe.

Katika mji wa San Bruno, jimbo la Californiua, Susan Susan Wojcicki, mkuu wa YouTube’s binafsi husimamia shughuli hiyo. Na kule Menlo Park, maafisa waandamizi ndiyo huendesha kitengo cha “Content Standards Forum” kinachosimamia miongozo ya kimaadili inayotakiwa katika jumbe zinazosambazwa kwenye mtandao wa facebook. Kitengo hicho ndicho kimetokea kuwa ni sehemu kuu ya mtandao huo kujitangaza kwa wanahabari.

Wasimamizi wa kitengo hicho hupendekeza miongozo mipya kuhusu kipi kifanyike kuhusu, kwa mfano, picha inayowaonyesha wanwaamke wa Kihindu wakipata mkong’oto nchini Bangladesh ambayo inaweza kuchochea ghasia katika jamii. Picha ya aina hii huondolewa. Lakini video inayoonyesha ukatili wa polisi wakati ghasia za kibaguzi wa rangi nchini Marekani huachwa mtandaoni.

Hali kadhalika, picha inayoonyesha Donald Trump, katika miaka ya 1990 akivaa magwanda ya kikundi cha Ku Klux Klan, kikundi cha kibaguzi cha watu weupe hupendekezwa ibakie mtandaoni lakini wanaotumia mtandao wajulishwe kwamba picha hiyo ni feki.

Maamuzi yanayofanywa kwenye vikao hivi mwishowe hutiririka kama maagizo kwa maelfu ya wasimamizi wa mitandao waliozagaa duniani kote.

Kuona tu kwamba kila kamouni ya mtandao wa kijamii husimamia na kurekebisha yale yanayowekwa kwenye mitandao yao ni kitu cha kutia moyo. Mitandao hiyo miwili, Facebook na YouTube haichukulii kazi hiyo kama shughuli ya ziada tu, bali ni mazoezi muhimu katika biashara yao.

Kila kampuni huajiri maafisa waandamizi ambao ni makini katika kazi ya kuifanya mitandao hiyo ya kijamii kuwa rafiki zaidi, lakini pia wakilinda uhuru wa kujieleza na wa kupata habari.

Hata hivyo shughuli hii wanayofanya pia ni suala la kutia wasiwasi, kwani hawa watu wanaelekea kujifanya wao kuwa ni “wasimamizi wa ukweli” kwa dunia nzima. Haijawahi kutokea – idadi ndogo sana ya makampuni yamekuwa na uwezo mkubwa kudhibiti kile mabilioni ya watu duniani wanachokisema au kukiangalia.

Na kwa upande wao wanasiasa kote duniani wanazidi kufuatilia kile kinachosheheni katika mitandao hii ya kijamii, kwa kuzingatia sera wanazotumia kukitathmini.

Wiki iliyopita (Septemba 5) Sheryl Sandberg ambaye ndiye mwendeshaji mkuu (chief operating officer) wa mtandao wa Facebook na Jack Dorsey, bosi wa Twitter, walihojiwa na Kamati maalum la Bunge la Senate la Marekani kuhusu ni mitandao ipi ya kijamii ndiyo inahusika sana katika kuruhusu maafisa wa kijasusi wa Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani wa 2016.

Basadaye Dorsewy (wa Twitter) alilazimika kujibu maswali makali kutoka Kamati ya Bunge la wawakilishi kuhusu urekebishaji ya yanyoshehenikatika mtandao wake.

Hata hivyo katika kikao cha awali cha mahojiano, kampuni ya Alphabet inayomiliki Google na YouTube iliwakilishwa na kiti kitupu baada kukataa kumruhusu Larry Page, mmoja wa waasisi wake kuhudhuria kikao hicho.

Uchunguzi kwa mitandao ya Facebook, Twitter, YouTube na mingineyo umeongezeka sana katika siku za karibuni. Mitandao yote hiyo mitatu inakabiliwa na wito wa kumfungia Alex Jones mtayarishaji wa kipindi cha Infowars kinachoelezea masuala mengi kuhusu ‘njama. zinazosukwa sehemu mbali mbali duniani. Hatimaye Facebook na YoutTube zilifanya hivyo.

Na wakati huo huo mitandao hiyo imakuwa ikikabiliana na tuhuma za uipendeleo dhidi ya uhafidhina kwa kugandamiza habari fulani fulani. Mtuhumu mkuu katika hili ni Rais Donald Trump, ambaye ametishia, kupitia akaunti yake ya Twitter kuisimamia.

Kwani baada tu ya mahoijiano na kamati za Bunge, Jeff Sessions, Mwanasheria Mkuu alisema atashauriana na wanasheria wakuu wa majimbo mengine kuhusu ya kile alichokiita ‘kuongezeka kwa wasiwasi” namna mitandao ya kijamii inavyotibua ubadilishanaji huru wa mawazo.

Haya yanayojiri yanaashiria mwisho wa kinga maalum ya kisheria iliyokuwapo kwa mitandao hiyo ya kijamii nchini humo. Nchini Marekani makampuni ya Intaneti yana kinga ya kisheria kwa kie kinachwekwa kwenye huduma zao wanazotoa.

Makao Makuu ya Facebook, Menlo Park , California.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.