Heri ya kuzaliwa Rais Magufuli

Rai - - MAKALA - Abbas Mwalimu. +255 719 258 484, Uwanja wa Diplomasia.

HONGERA Rais Dk. John Magufuli kwa kutimiza miaka 59 tangu kuzaliwa kwako. Mungu azidi kukupa nguvu zaidi, siha njema na maarifa zaidi katika kuwatumikia watanzania.

Nahisi hatukukuelewa ulipotusisitiza watanzania tuzaane kwa wingi. Miongoni mwa mambo ambayo Rais Magufuli amekuwa akiyasisitiza ni kuhusu watanzania kuzaana kwa wingi.

Mara ya kwanza alitoa kauli ya kusisitiza kuzaana pale Dodoma Makutupora wakati wa akizindua mradi wa reli ya kisasa ya SGR.

Kwa kuonesha msisitizo alirejea kauli yake kule Geita. Msisitizo huu sisi watu wa uhusiano wa kimataifa tunauelewa, lakini hatuna hakika kama jamii inauelewa.

Ili kufahamu kwa nini Rais anasisitiza hili tupate rejea:

Mwaka 1975 aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani na Mshauri wa Mambo ya Usalama wa Marekani, Henry Kissinger miaka ya 1960, alizuru nchini China.

Baadae mwaka 2011 aliandika kitabu alichokiita “On China”. Katika kitabu hiki Henry Kissinger alielezea kwamba China itakuja kuwa Dola lenye nguvu zaidi.

Kwa nini?

Henry Kissinger alianisha sababu, akasema:

(1) China ina eneo kubwa (Territory)

(2) Ina idadi kubwa ya watu (Population) (3) Ina rasilimali za kutosha (4) Inakuja juu katika teknolojia

Na sababu nyingine kadhaa; Chatterjee Aneel (2010:) katika kitabu chake International Relations Today: Concepts and Application ameeleza viashiria vinane vya dola kuwa na nguvu: (1) Geography (2) Population (3) National Resources (4) Popular Support (5) National Character (6) Technology and Military strength (7) Ideology and (8) Leadership Aneel (2010:59) Kwa kutazama vigezo hivyo kigezo cha idadi ya watu (population) ndicho hupelekea hayo mengine yote kufikiwa kwa kiwango kinachotakiwa, je tunazaana?

Nafahamu wapo watakaoleta nadharia ya Malthus, lakini bado kwangu umuhimu wa population utabaki kuwa namna gani hiyo idadi ya watu inatumika na si kupinga idadi ya watu.

Kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia, Ujerumani yenye kilometer za mraba 357,386 ina watu milioni 82.52 wakati Tanzania yenye kilometer za mraba 945,087 ina idadi ya watu milioni 57.31.

Kwa hesabu za haraka kulinganisha ukubwa, nchi gani ilipaswa kuwa na idadi kubwa ya watu?

Heri ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli. Nahisi hatukukuelewa ulipotusisitiza watanzania tuzaane kwa wingi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.