Mikopo inavyozidi kulipeleka Afrika katika shimo la umasikini

Rai - - MAONI/KATUNI - NA ELIYA MBONEA, ARUSHA

Baada ya Donald Trump kuingia madarakani, mambo mengi yamebadilika katika maeneo tofauti tofauti duniani. Marekani ya sasa haijaipa kipaumbele Afrika. Marekani ya sasa imejikita katika barani Asia na kupunguza uhusiano wake kwa kiasi fulani

BODI ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) imemaliza muda wake wa miaka minne tangu ilipoteuliwa na Rais Dk. John Magufuli Septemba 22, mwaka 2015.

Chini ya Mwenyekiti Meja Jenerali mstaafu Hamis Semfuko na wajumbe wake, walikabidhiwa majukumu ya kuhakikisha Taasisi hiyo nyeti ya uhifadhi inasimama, kujiendesha na kuchangia uchumi wa Taifa.

Meja Jenerali Mstaafu Semfuko aliyetumika jeshini kwa miaka 40, anamshukuru Rais Dk. Magufuli kwa kumwamini na kumteua kutumika kwenye nafasi ambapo anajivunia mafanikio yaliyofikiwa.

Anasema bodi hiyo imekuwa ya kwanza kutokana na kupewa majukumu ya kuanzisha Shirika lililopewa majukumu mazito yaliyosimamiwa awali na Idara ya Wanyamapori kama Idara ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mamlaka hiyo kisheria inasimamia eneo la takribani asilimia 20 ya nchi likiwa na Mapori ya Akiba, Tengefu yenye vitalu vya uwindaji wa kitalii takribani 170 na maeneo oevu.

Anasema baada ya kuona maeneo hayo kwa kiwango kikubwa wanyama wanapotea kupigwa, kuuawa na majangili serikali iliona muhimu wa kuanzisha TAWA ili isimamie rasilimali kwenye maeneo hayo.

“Kazi kubwa imefanyika ya kuhakikisha kunakuwa na makabidhiano kutoka Idara ya wanyamapori ilituchukua muda lakini tulifanikiwa.

“Tulianza kazi Julai Mosi, mwaka 2016 tukiwa na mtaji mdogo wa Sh milioni 350, maeneo tuliyopewa kusimamia yalikuwa na hali mbaya ya kiuhifadhi.

“Eneo kama Pori la Akiba Selous idadi ya tembo iliporomoka na kufikia 15,000, hii nayo ilikuwa sababu iliyofanya Serikali kuanzisha TAWA, ili itumie zaidi weledi, maarifa na kuhakikisha wanyamapori hawapotei.

“Nina furaha kusema eneo hilo ambalo mwaka mzima ilikuwa si ajabu kuokota mizoga ya tembo isiyopungua 17 mpaka 20 inayoonyesha kuuawa kwa ujangiri.

“Sensa iliyopita tumepata mizoga ya tembo mitano tu hii ni moja ya faraja kwetu kwasababu haya ni mafanikio makubwa katika uhifadhi,” anasema Mwenyekiti wa huyo.

Kutokana na miongozo ya uhifadhi iliyotolewa na Rais Dk. Magufuli kwa bodi hiyo anasema, imewezesha Tembo kuongezeka na hadi kufikia hatua ya kutoka nje ya maeneo ya hifadhi kutokana na kutohofia kuuawa.

“Woga wa wanyama kuwindwa haupo ndio maana ongezeko lao linakwenda mpaka nje ya maeneo ya hifadhi, wanyama wamekuwa na uhuru wa kutembea,” anasema Mwenyekiti wa Bodi

Kuhusu mapato yatokanayo na shughuli zinazosimamiwa na TAWA, Meja Jenerali Mstaafu Semfuko anasema,maagizo ya bodi kwenda kwa menejimenti ya Taasisi hiyo ni kuhakikisha wanaongeza mapato.

“TAWA imekuwa na uwezo mkubwa imeanza kujiendesha wamefikia Sh bilioni 47 kwa mwaka. Maagizo yetu wahakikishe wanaongeza mapato tumewataka wafikie malengo ya Sh bilioni 100 ifikapo mwaka 2021,” anasema.

Akielezea mafanikio waliyopata kwa kipindi chao kama Bodi ya TAWA anasema, wakati wa ziara yao ya kwanza waliwahi kukuta askari wakiwa wamevaa kandambili na kipande cha hema wakiwa doria.

“Leo tunajivunia kuona askari wetu wakiwa na mavazi safi viatu na vitendea kazi imara kabisa, kwani tumenunua magari takribani 77 ili kusaidia uhifadhi kwenye mapori yetu.

“Tumejenga maghala ya kuhifadhia silaha, bunduki inahitaji utunzaji mzuri isipotunzwa inaweza kuleta madhara. Hili lilikuwa moja ya malengo yetu kuona maghala ya kutunzia bunduki na risasi yanajengwa.

“Tupo kwenye mkataba wa kwanza tumewapa JKT watujengee maghala 18, lakini pia mpango mkakati wetu ni kuongeza mapato zaidi kuitia zao jipya la utalii wa uvuvi wa samaki,” anasema Meja Jenerali Mstaafu Semfuko.

Anasema mbali ya kumaliza muda wake Bodi imetoa maagizo kwa menejimenti ya TAWA ikiwataka viongozi na watumishi kuendelea kubadilika.

“Bodi imefanya kila juhudi za kuwabadilisha ili wawe wazalendo zaidi,wafanye kazi zao kwa weledi. Hili ni shirika kubwa wanapaswa kuondokana na matatizo yanayoweza kuwatia doa,” anasema.

Mratibu wa shughuli za uwindaji wa kitalii Kampuni ya Mkwawa Hunting Safari katika Pori la Akiba Selous, Benson Kibonde anasema uwindaji huo ulianza miaka mingi una faida za Kiikolojia, kiuchumi, utamaduni na kijamii.

Akielezea faida za kiuchumi anasema, Tanzania inachukua nafasi ya pili Afrika kwa kuwa na mapato makubwa yanayotokana na utalii wa uwindaji wa kitalii ikitanguliwa na Afrika Kusini.

“Tanzania inakadiriwa kufikia mapato ya takribani dola za Marekani milioni 60 hizi ni fedha nyingi hasa ukiangalia idadi chache ya watu wanakuja kufanya utalii wa uwindaji,” anasema Kibonde.

UWINDAJI NI UHIFADHI

Anasema shughuli za uwindaji zinapofanyika huwa ni sehemu ya uhifadhi kwani huwezesha kufika maeneo mengi na kama kuna hatari inakuwa rahisi kuwasiliana na TAWA ili kuleta wataalamu zaidi.

“Kwa miaka yote tangu tuingie hapa ujangili umeshuka, tuna vyombo vya maji (boti), kwa ajili ya doria na magari ya kutosha.

“Na kitaalamu kabisa ni kwamba ukifuta uwindaji wa kitalii hakika madhara yatakuwa makubwa kwenye maeneo yaliyohifadhiwa, yapo maeneo ambayo uwindaji ulipoondolewa yalivamiwa na mifugo na wakulima na hatinmaye kuondoa uoto wa asili na uhifadhi,” anasema Kibonde.

Anazitaja faida za kijamii zinazotokana na uwindaji wa kitalii kuwa ni pamoja na misaada mbalimbali ya ujenzi wa shule, hospitali ofisi za vijiji vilivyo jirani na mapori ya akiba.

Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA Meja Jenerali Hamis Semfuko akipokea heshima wakati wa moja ya ziara zake za kutembelea Pori la Akiba Maswa, lililopo mkoani Simiyu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.