Mikopo inaipeleka Afrika katika shimo la umasikini

Rai - - MAKALA - Itaendelea wiki ijayo NA MPOKI BUYAH

BAADA ya Donald Trump kuingia madarakani, mambo mengi yamebadilika katika maeneo tofauti tofauti duniani. Marekani ya sasa haijaipa kipaumbele Afrika. Marekani ya sasa imejikita katika barani Asia na kupunguza uhusiano wake kwa kiasi fulani katika na mataifa ya Afrika ndani ya miaka miwili ya utawala wa chama cha Republican na kujikita kwenye itikadi yake yake ya ‘Make America Great again’ (America First the rest will follow).

Bwenyenye huyo amekuwa akiyanyoshea vidole mataifa ya Afrika kwa uongozi usiothabiti na alienda mbali zaidi, kwamba mataifa ya Afrika yananuka kama choo. Hapa alikuwa analenga uongozi mbaya na usiojali wananchi wake.

Hata hivyo, mke wa Trump, Melanin Trump ametembelea Kenya Oktoba 4 mwaka huu akitokea Ghana na Misri pia alitembelea mji wa Giza kuangalia Pyramids. Pia alitembelea Malawi, mataifa yote haya ni wanufaika wakubwa wa Marekani hususani Kenya na Misri wamekuwa na uhusiano wa karibu ndani ya miaka hii ya karibuni.

Kupungua kwa ushawishi wa Marekani kumeifanya Afrika ikimbilie China katika kujiendesha ila usisahau kwamba mfadhili mkubwa wa bara la Afrika bado ni Marekani na siyo China.

Afrika katika ulimwengu wa China, ni muda wa miaka 20 sasa tangu Bara la Afrika kuanza kupokea mikopo na msaada kwa kiasi kikubwa kutoka China, Bara la Afrika linafungua ukurasa mpya katika kujiingiza katika shimo la madeni kutoka China pasipo kujua namna gani wataweza kurejesha mikopo hiyo.

China imehusika katika miradi mbalimbali ya barani Afrika, kujenga viwanja vya ndege, barabara za kisasa, madaraja makubwa, uwekezaji katika nishati ya umeme na katika uwanja wa mawasiliano kurahisisha ukuaji wa uchumi na huduma za kijamii lakini unakuwa ni mzigo mzito katika kulipa madeni hayo miaka 10-30 ijayo.

Kwa upande wa Afrika mashariki pekee mpaka sasa kulingana na taarifa kutoka taasisi ya CARI (China African Research Initiatives), China imekopesha zaidi ya dola za Marekani bilioni 29.42 huku Kenya wakiwa wamechukua kiasi kikubwa kuliko mataifa mengine Afrika mashariki na kati.

Wasiwasi umeibuka miaka ya karibuni juu ya mikopo isiyokuwa na riba kutoka China na hili sakata la Zambia kuingia katika mkwamo na kutawaliwa upya kwa mara ya pili na serikali ya China.

China ndiyo muwekezaji mkubwa nchini Zambia, China amejenga vituo vya polisi nchi nzima, asilimia 90 ya barabara zimejengwa na China, kwenye upande wa ujenzi wa viwanja vya mpira, uwanja wa ndege na pia kwenye upande wa nishati mchina ndiyo amewekeza huko.

Zambia ametawaliwa na China, Zambia hakuna wanachoweza kufanya pasipo kupata maamuzi kutoka China, Zambia siyo taifa huru tena kama zamani, mpaka sasa Zambia wamekopa dola za Marekani bilioni 13, lakini pia Taifa hilo limekuwa likificha uhusiano na China ingawa kuna taarifa zinaenda mbali zaidi kwamba kuna uwezekano mkubwa wakawa wanadaiwa dola za Marekani bilioni 30 ambazo kwa lugha nyepesi Zambia hawawezi kulipa mali pesa zote hizo hivyo kupelekea mashirika na mali nyingi za Zambia kiwa chini ya China.

Mikopo ya China inaenda kuliingiza Bara la Afrika katika umasikini wa kudumu endapo viongozi wetu hawatachukua hatua za mapema katika kuandaa mazingira ya ulipaji madeni hayo.

Afrika pia imetembelewa tayari na Rais wa China, Xi Jipping Rais huyu wa milele kutoka China ambaye anapewa heshima sawa na Mao Tse Tung (Mao Zedong) mwasisi wa taifa hilo. China amewekeza sana Afrika kuliko sehemu nyingine yotote ile duniani na mataifa ya Afrika yananufaika sana na China katika miundombinu na teknolojia miaka ya karibuni hilo halina ubishi hususani katika mikopo isiyokuwa na riba ambapo mpaka sasa mikopo ya China imeanza kuogopesha na kutia wasiwasi maana mataifa ya Afrika yanazidi kujitumbukiza kwenye shimo la umasikini. Maana wanakopa lakini namna ya kurudisha mikopo hiyo imekuwa changamoto maana mataifa ya Afrika yanachukua mikopo kutoka China huku wakitegemea kurudisha mikopo hiyo kwa kodi za watu masikini.

Afrika Kusini ni moja ya taifa linalopekea msaada mkubwa wa mikopo usiyokuwa na riba kutoka China bila kusahau Ethiopia ambao kulingana na China African Research initiatives ndani ya miaka ya karibuni Ethiopia pekee imekopa dolami bilioni 13.73 katika ujenzi wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa reli za kisasa (SGR), ambayo pia ujenzi unaendelea kutoka mji mkuu wa Adis Ababa kwenda Djibouti. Na ujenzi huo utagharimu dola za Marekani bilioni nne pekee, taifa la Ethiopia liliweka rekodi ya kuwa taifa la kwanza kuchukua mkopo mkubwa ndani ya mwaka 2013 .

Miradi mingi inayofanyika Ethiopia ni pamoja na mikopo kutoka China ila wachuuzi wa mambo wanadai kwao wao wanaweza kulipa mikopo hiyo pasipo shida yoyote ile na hii ni kutokana na aina ya uchumi walionao tofauti na mataifa mengine kama Uganda, Sudani, Zambia na Tanzania. China imehusika katika kujenga miradi mikubwa ya umeme chini humo hata hivyo taifa litalazimika kuwabana watu wake katika kulipa kodi ili kurudisha madeni hayo lakini bado kuna wasiwasi kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kushindwa kulipa madeni hayo kwa China ndani ya miaka 1020 ijayo na kujitumbukiza kwenye mkwamo wa madeni.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.