KIMATAIFA: MIKOPO INAVYOZIDI KUIPELEKA AFRIKA KATIKA SHIMO LA UMASIKINI

Rai - - MBELE - NA MPOKI BUYAH

Wnamna IKI iliyopita tulidadavua

Bara la Afrika lilivyoanza kupokea mikopo na msaada kutoka China zaidi ya miaka 20 iliyopita na kufungua ukurasa mpya wa kujiingiza kwenye shimo la madeni pasipo kujua namna gani wataweza kurejesha mikopo hiyo. Endelea…

Kenya hawako nyuma

kwenye mikopo ya China kwani wanadaiwa zaidi ya Dola za Marekani bilioni 9.8, na hizo ni zile ambazo wamechukua miaka ya karibuni kwa ajili ya miundombinu ya kisasa pamoja na nishati lakini sana katika ujenzi wa reli mpya za kisasa mfano wa ile inayojengwa kutoka Naivasha kwenda Kisumu ambayo itagharimu zaidi ya Dola za Marekani bilioni3.8 kutoka China.

Hata hivyo, kulingana na uchumi wa taifa hilo wamejigamba kwamba wanaweza kulipa deni ingawa Kenya na Ethiopia ni miongoni mwa nchi zenye kuonesha wasiwasi kama zitaweza kulipa madeni hayo kutoka China ambayo yanaonekana kuliingiza bara la Afrika umasikini mkubwa.

Uganda pia hawako nyuma katika kukopa kutoka China, ndani ya miaka mitatu tangu mwaka 2015/2018 Uganda wamechukua mkopo kutoka China kiasi cha Dola za Marekani bilioni 2.96 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kisasa inayotoka Entebe kwenda Kampala ambayo kwa kiwango kikubwa imekamilika na inaonekana kuanza kifanya kazi.

Wasiwasi umeibuka pia iwapo Uganda itaweza kukusanya mapato ipasavyo na kurejesha mkopo huo maana imeonekana wazi kwamba Uganda ni moja ya mataifa ambayo yapo nyuma sana katika ukusanyaji wa mapato Afrika mashariki na kati ukiachilia mbali DRC na Sudani Kusini ambao wamekopa katika kujenga barabara zinazosaidia uwekezaji kwenye nishati. Mpaka sasa wapo vitani, haijulikani watalipa lini hizo hela za Wachina.

Kuongezeka kwa ushawishi wa China barani Afrika hakuna ubaya wowote ila kumekuwa na faida kubwa kwenye sekta ya miundombinu na nishati tangu mwaka 2000 mpaka sasa, mikopo ya China imetufuta machozi kwa kiasi fulani katika nyanja mbalimbali ila pia ni vyema kutambua kwamba mikopo hii tusipojitambua vyema itakuja kutuletea shida kubwa na kuendelea kuwa watumwa hapo baadae.

Viongozi wa Afrika wahakikishe kwamba Waafrika wananufaika pakubwa na uwepo wa China barani Afrika lakini pia wahakikishe wanachukua mikopo ambayo watakuwa na uwezo wa kulipa nje ya hapo wajiandae kuwa watumwa wa China kifikra na kiuchumi miaka 20 baadae kwani dalili zimeanza kuonekana Zambia.

Tusifurahie mabilion ya pesa yanayamwagika Afrika kutoka China ila ni vyema pia mikopo hiyo iwe na faida kwa pande mbili maana kinachoonekana mikopo ya China ambayo haina riba imeanza kuwa tishio kwa Afrika.

Hii inatokana na kuwa na mikakati mibovu juu ya ulipaji madeni hayo wakati China ukishindwa kurejesha pesa zao wanatabia ya kushika miundombinu kama viwanda, viwanja vya ndege, migodi, barabara ama kitu chochote kitakachorudisha hela yao.

Haya yametokea Burma (Mynmar), Malysia, Sri Lanka na kwa upande wa Afrika- Zambia yamewasha taa nyekundu hawawezi kufanya chochote pasipo kuihusisha China bila kuwasahau Angola.

Tutaendelea kukamuliwa mpaka ibaki mifupa endapo hatutakuwa makini na mikopo ya China na mataifa makubwa. Uwepo wa China -Afrika umeonekana kutiliwa shaka miaka ya karibuni tofauti na miaka ya 1990s.

Mataifa mengi yamemkaribisha Mchina Afrika kwa sababu mikopo yake isiyokuwa na riba, amekuwa msaada mkubwa katika miundombinu lakini mikopo hiyo imeonekana kuzielemea nchi nyingi za Ki-Afrika.

Xi ametembelea mataifa mengi zaidi Afrika kuliko taifa lolote lile kubwa duniani miaka ya hivi karibuni. kuanzia mwaka 2012- 2018, Xi ametembelea Senegal, Afrika kusini, Rwanda, Sudan na mataifa makubwa mengine na yote hiyo ni katika kuimarisha biashara na uhusiano wa kidiplomasia. China amekuwa na msaada mkubwa katika maendeleo ya Afrika ila mikopo yake isiyokuwa na riba pia imekuwa kikwazo maana mataifa mengi ya Afrika yanakopa lakini hayazalishi chochote na hii kujikuta wana malimbikizo ya mikopo isiyokwisha.

Utafiti wa taasisi ya Afrika Institute Researh kutoka Chuo kikuu Marekani ulionesha kuwa kuanzia mwaka 2000 mpaka 2018 China imekoposha dola zaidi ya billion 143 katika bara la Afrika. Mikopo imekuwa kutoka Dola za Marekani billion 5 hadi billion 30 ndani ya mwaka 20162017, mikopo yote hiyo imekuwa ikikua kila siku na mataifa ya Afrika yameonekana kutokuwa na uwezo wa kurudisha mikopo hiyo na hiyo hupelekea mataifa ya Afrika kuwa vibaraka na watumwa wa mikopo.

Angola pekee ndiyo limekuwa taifa ambalo linalonufaika pakubwa na mikopo kutoka China, kwa muda wa miaka 17 kuanzia mwaka 20-2018, taifa hilo limekopa dola billion 42 kwa mujibu wa China African Research Iniatiative. Huku Zambia wakiwa wamekopa dola billion 13 japokuwa inasemekana Zambia inadaiwa zaidi ya Dola za Marekani bilioni 20 ila wanaficha na Serikali hiyo ipo katika mkwamo wa kulipa madeni hayo na hivyo kupelekea baadhi ya mali za Serikali kushikiliwa. Lakini Zambia mekanusha ingawa ndio uhalisia wa Afrika katika mkwamo wa madeni kutoka nje.

Septemba 3, mwaka huu mataifa zaidi ya 50 yalikwenda China kushiriki mkutano mkuu baina ya China na Afrika FOCAC (Forum China-Afrikani Cooperation), kulingana na Jarida la Afrika Fundamental ni kwamba China ameahidi mataifa ya Afrika kutoa mkopo wa dola billion 60 katika mataifa zaidi ya 50 kuanzia sasa na kuendelea.

Bado tunaendelea kukopa na hapo ndipo wazungu wanasema Xi ‘has played his Card Right’. Mataifa karibia 50 ya Afrika yanategemea msaada kutoka mataifa wahisani, 60% ya bajeti nyingi za mataifa ya Afrika hutegemea pesa kutoka nje.

Tunakaa bungeni na kupanga bajeti kubwa lakini unakuta hatuna hela kwani ni mpaka tuanze kuomba msaada kutoka Uingereza, Ujerumani au Ufaransa na Marekani huku yale mataifa ambayo ya Afrika ambayo hayajamaliza mikopo ya Marekani, yamehamia kukopa China. Tunapanga mambo mengi na kutoa ahadi nyingi wakati hela zenyewe za mikopo. 0762155025, Email:mpokibuya@ gmail.com

Ujenzi wa reli ya kisasa ukiendelea.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.