Mwananchi asimulia alivyosam Muhimbili mkewe alipojifungu

Uhuru - - Afya Na Mazingira - NA SIMON NYALOBI

EKTA ya afya ni miongoni mwa sekta muhimu kwa maisha ya Watanzania, ambayo huwahakikishia usalama wa maisha yao. Katika kipindi cha mwaka mmoja, tangu serikali ya awamu ya tano, ilipoingia madarakani chini ya Rais Dk. John Magufuli, imefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya afya. Baadhi ya wananchi katika makala hii wanazungumzia mafanikio na changamoto kwenye sekta ya afya katika kipindi cha mwaka mmoja tangu alipoingia madarakani. Wananchi wanazungumzia namna walivyofurahishwa kwa namna ambavyo serikali imefanya mageuzi makubwa kwenye sekta hiyo ikiwemo uboreshaji wa mashine za vipimo na vifaa tiba. Lakini pia wanaelezea changamoto changamoto ambazo zimejitokeza kwenye sekta ya afya ambazo bado ni kero. Mkazi wa Sinza kwa Remmy, Sudi Chambela (35), anasema Rais Magufuli amejitahidi kurudisha imani ya wananchi katika huduma za afya hususan kwenye hospitali za umma. Anabainisha kwamba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) huduma zinazotolewa zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa na ufanisi umeimarika. Chambela akiwa katika hospitali hiyo ambako alimsindikiza mkewe kupata matibabu na wanawe watatu ambao ni mapacha. “Watoto wangu walizaliwa miezi mitatu iliyopita hospitalini hapa, kilichonifurahisha ni namna huduma zinavyotolewa. Wananchi wa kawaida watunyanyasiki tunahudumiwa vizuri,”anaeleza. Chambela anasema kwamba mkewe alijifungua mapacha watatu katika wodi ya wazazi hospitalini hapo, ambapo ili kuondoka na mkewe na watoto wake ingemlazimu kulipa kiasi kikubwa cha fedha ambacho alikuwa hana wakati huo.

“Nashukuru Mwenyezi Mungu baada ya Rais Magufuli kutembelea hospitalini hapa kulitusaidia. Hivi sasa huduma za afya ni mzuri, mimi mwenyewe sijui ningefanyaje sababu mke wangu alijifungua kwa oparesheni,

Kwa kawaida ukijifungua kwa oparesheni ni lazima ulipie sh. 300,000, hivyo kwa vile mke wangu alijifungua watoto watatu nilitakiwa nitoe sh. 540,000 ikiwa ni gharama za mama na watoto,”anaeleza.

Lakini anaeleza kwamba alipata msamaha wa kutolipa gharama hizo kwa ruhusa ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Anasema Ummy alitoa msamaha huo wakati akitekeleza agizo la Rais Magufuli la kupeleka vitanda katika wodi ya wazazi.

Chambela anasema hali ilivyokuwa miaka ya nyuma katika hospitali hiyo ni tofauti na ilivyo sasa kwani kipindi hicho wajawazito walikuwa waliteseka na kupelekea kuwakana waume zao.

“Ilifikia wakati wanawake wanakuja kujifungua lakini wanasema hawajaolewa ili wahurumiwe kutozwa gharama za kujifungua, lakini hali hiyo ni tofauti hivi sasa,” anasema.

Kuhusu kuwepo kwa vitanda, Chambela anasema agizo la Rais Magufuli la kupelekwa vitanda katika hospitali hiyo limesaidia na kwamba hivi sasa hakuna mgonjwa anayelala chini.

Hata hivyo anasema baadhi ya wauguzi katika hospitali hiyo wanataka kurudisha nyuma jitihada za serikali ya awamu ya tano, kwa kuendelea kutoa huduma chini ya kiwango wakati wakiwahudumia wagonjwa.

Akizungumzia gharama za upasuaji kwa wazazi wanaojifungua, Chambela anaiomba serikali kupunguza gharama hizo na kufikia sh. 100,000 au 50,000 ili wananchi wa kipato cha chini waweze kuzimudu.

“Kwa mtazamo wangu serikali kwa sasa inatakiwa kuboresha huduma za upatikanaji wa dawa, kupunguza gharama za matibabu ili kuwawezesha wananchi wengi kuzimudu gharama hizo,” anasema.

Lakini Sufiani Hassan, ambaye alifika kupatiwa matibabu ya meno na fizi katika hospitali hiyo anasema huduma zinazotolewa zinaridhisha tofauti na ilivyokuwa mwanzo.

Anasema baada ya Rais Magufuli kutembelea ho hiyo, wauguzi na madaktari wanafanya kazi kubwa n uadilifu.

Hassan anasema kitengo cha huduma za kinyw meno kinatoa huduma mzuri na kwamba wauguzi utaratibu mzuri wa kuwahudumia wagonjwa.

“Hivi sasa huduma katika hospitali hii ni mzu madaktari wapo wengi na wanatuhudumia vizuri, hata foleni kama unavyoona hapa si ndefu kwa sa wagonjwa wanahudumiwa na wanaondoka mape anasema.

Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Kinywa na Mata MNH Dk. Jeremiah Moshy, anasema ziara ya Rais Ma hospitalini hapo, imeleta mafanikio makubwa.

“Tangu Rais Magufuli alipokuja hapa, hakuna mtu anayefanya kazi kwa mazoea, kila mmoja wetu anatek majukumu yake bila kusimamiwa,” anasema.

Dk. Moshy anasema hatua zilizochukuliwa na Magufuli zimesaidia kurudisha misingi ya uwajibikaj wafanya kazi wa sekta ya afya nchini na kwamba ha ikiendelea itazidi kuboresha sekta ya afya.

“Katika kipindi hiki cha mwaka mmoja cha uongo serikali ya awamu ya tano kwa kusema kweli ume vizuri kwenye sekta ya afya kwani inaendelea kuim kila siku. Hata hapa Muhimbili baada ujio wa Rais m yanakwenda vizuri,” anasema.

Anaongeza kuwa “Rais Magufuli ameonyesha m na uhakika wa kubadilisha hali, hivyo mambo me madogo madogo yanaweza kuondoka. Unajua wanataka kila tatizo lililopo hapa Muhimbili lio wakati huo huo haiwezekani.”

Dk. Moshy ambaye ni bingwa wa masuala ya up wa magonjwa ya kinywa, anasema changamoto iliyo uhaba wa vifaa hususan vya upasuaji katika vyumb wagonjwa mahututi (ICU).

Anasema idadi ya wagonjwa wanaofika hospitalin ni wengi, hivyo uhaba wa vifaa vya upasuaji unasaba kuzorota kwa huduma na kusababisha malalamiko.

Dk. Moshy anasema wagonjwa wanaofika hosp hapo, wengi ni wa kipato cha chini, hivyo kuwatoza gha za upasuaji ikiwemo vifaa itasababisha washindwe k matibabu.

Mkurugenzi wa Shirika la Utetezi wa Masua Afya kwa Wanawake na Wasichana (KIWOHEDE) Mwaituka, anaipongeza serikali ya awamu ya tano k kurudisha nidhamu ya uwajibikaji katika hospita serikali.

Justa anasema kwa sasa wahudumu wa afya wa ushirikiano kwa wagonjwa tofauti na ilivyokuwa.

“Katika hospitali zetu wauguzi wanawaona wago kama washirika wao na si wahitaji wa huduma, h kwa kweli ni jambo la heri na ni mabadiliko mak yaliyopatikana kwenye sekta ya afya,”anasema.

Anaishauri serikali kuhakikisha inawapatia hudu bima ya afya watoto walioko katika makundi maalu wapate huduma bila kupata usumbufu hospitalini.

Justa anasema watoto walio kwenye makundi maa wanakabiliwa na changamoto za ubaguzi wanap hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Naye Ofisa Programu wa Mtandao wa Jinsia Tan (TGNP), Deogratias Temba, anasema serikali ya a

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.