Watumishi wa umma wadaiwa kukwepa kujisajili NIDA

Uhuru - - Mbele - NA WILLIAM SHECHAMBO, DODOMA

MAMLAKA ya Usimamizi wa Usafiri wa Anga (TCAA), inatarajiwa kuhojiwa wiki ijayo na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Kampuni ya Ndege ya Fastjet.

Hayo yalibainika jana, mjini hapa, baada ya wajumbe wa kamati hiyo, kutaka kumuuliza maswali Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuhusu kampuni hiyo.

Profesa Mbarawa aliwataka wajumbe hao wawe na subiri kwani Oktoba 26, mwaka huu, mamlaka hiyo itafika mbele ya kamati na watauliza maswali.

“Waheshimiwa yatunzeni maswali yenu, mtayauliza tarehe 26, wakija watu wa TCAA,”alisema.

Wakati huo huo, kamati hiyo imeiomba serikali impeleke mafunzoni Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) nchini China na bodi yake mpya ili wakaongeze ufanisi katika kulifufua shirika hilo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Richard Sigalla, alisema mafunzo hayo ni yale yanayohusu biashara ya usafiri wa anga, ambayo Serikali ya China inayamudu vizuri kwenye biashara hiyo tangu ilipoanza ikiwa na ndege tatu, mwaka 1982 hadi leo, ambapo inazo ndege zaidi ya 2,300.

Sigalla alisema hayo jana, kwenye kikao hicho cha kamati, ambacho kiliialika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na baadhi ya taasisi zake.

Alisema serikali imeamua kulifufua shirika hilo kwa kununua ndege zake, kuunda bodi mpya na kumteua mkurugenzi mkuu mpya, hivyo haina budi kumpeleka kwenye mafunzo ya biashara pamoja na baadhi ya wajumbe wa bodi ili kushindana na soko.

Mwenyekiti huyo alisema vyuo vingi vinavyotoa mafunzo ya usafiri wa anga, havitoi elimu ya biashara ya ndege, hivyo ni ngumu sekta hiyo kukua haraka.

“Hatusemi kwa ubaya, isipokuwa ili tuliendeleze shirika letu, ipeni bodi mafunzo pamoja na mkurugenzi ili tuweze ushindani wa kibiashara, la sivyo utakuwa ni mtindo wa kutumbuana tu,” alisema.

Akijibu hoja hiyo, Profesa Mbarawa alisema wameichukua na wataifanyia kazi .

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.