Watumishi wa umma wadaiwa kukwepa kujisajili NIDA

Uhuru - - Habari -

SERIKALI imesema baadhi ya watumishi wa umma wamekuwa kikwazo katika uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa unaoendeshwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kwa kuogopa kujitokeza wakihofia kukutwa na nyaraka za kughushi.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, kuhusu mwenendo wa usajili wa vitambulisho.

Mwigulu alisema hiyo ni miongoni mwa changamoto kubwa iliyojitokeza wakati wa usajili wa watumishi hao.

Alisema usajili huo ulipaswa kukamilika Oktoba 17, mwaka huu, lakini haikuwa hivyo, kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwemo ya watumishi kutojitokeza kwa kuhofia kukutwa na nyaraka za kughushi.

Alizitaja changamoto zingine kuwa ni pamoja na wiki ya kwanza ya usajili kutumika zaidi kuandaa rasilimali watu na vifaa katika vituo vya kusajilia watumishi wa umma.

Changamoto nyingine zilizojitokeza ni watumishi wengi kujitokeza kujisajili tarehe za mwisho na taasisi nyingi zinazopata ruzuku ya serikali kuona watumishi hao hawahusiki katika mpango huo.

Hata hivyo, Mwigulu alisema NIDA tayari imesajili jumla ya watumishi wa umma 236,016, nchi nzima, ambapo miongoni mwao 110,237, tayari wameshapatiwa vitambulisho vya Taifa.

Alisema taarifa za wanaosajiliwa na kupatiwa vitambulisho hivyo, zitaunganishwa moja kwa moja na mfumo wa mishahara wa serikali, hatua ambayo itasaidia kuondoa changamoto ya malipo ya wafanyakazi hewa.

Waziri Mwigulu alisema idadi hiyo ni sawa na asilimia 51.05 ya watumishi wa umma waliokusudiwa kusajiliwa na NIDA.

Aliwataka waajiri wote kutoa ushirikiano wa kutosha kwa mustakabali wa uraia na utaifa, huku akiwataka walioshindwa kupata vitambulisho kutokana na sababu mbalimbali, kuwasilisha nakala ndani ya siku 14 baada ya kusajiliwa.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, akizungumza wakati wa kikao cha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari, mjini Dodoma, jana. (Picha na MAELEZO).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.