Maandamano sio msingi wa maendeleo

Uhuru - - Habari - NA MWANDISHI MAALUM

DHANA ya maendeleo si neno geni na limekuwa likisisitizwa kwa vitendo na viongozi mbalimbali hapa chini wakiwemo wa dini ambao kwa hakika wamekuwa wakirejea hata katika vitabu vitakatifu kuhusu umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii na uadilifu kwa maslahi ya umma.

Katika kipindi hiki sote tumeshuhudia kuwa dhamira ya Rais Dk. John Magufuli kuhakikisha kuwa wanyonge na masikini wa taifa hili wanafurahia matunda ya uhuru wa nchi yao kwa kujenga ari ya kufanyakazi na kutumia rasilimali zilizopo kujiletea maendeleo.

Ikumbukwe kuwa migogoro hutatuliwa kwa mazungumzo yanayofanywa kwenye vikao halali. Huu ndio utamaduni tuliojijengea kwa zaidi ya nusu karne.

Hii dhana ya kuiga eti kuleta suluhu kwa maandamano ni dhana potofu ambayo inabidi ipingwe kwa nguvu zote na kila mpenda amani.

Sote tunatambua athari za maandamano kwa kutumia mifano dhahiri ya nchi jirani mbazo zilitoa nafasi kwa wale wasiopenda amani kufanya vitendo vilivyopelekea kupotea kwa amani katika nchi hizo.

Je, wale mnaotuhamasisha vijana tuandamane mmemuelewa Rais kuhusu dhamira yake ya kutaka kila Mtanzania afanye kazi na kuachana na mambo yasiyo na tija ikiwemo maandamano, kukaa vijeweni nk.

Sijawahi kusikia popote duniani nchi iliyofikia maendeleo kwa sababu wananchi wake walifanya maandamano na vitendo vinavyofanana na hivyo, bali siri ya mafanikio ni kutumia muda vizuri kwa kufanya kazi vizuri ndipo tutaweza kuonyesha ulimwengu kuwa sasa dhamira yetu ni kujiletea maendeleo.

Lazima tujiulize kuwa China, Ulaya, Marekani na kwingineko wamefikia maendeleo ya kweli kwa sababu ya maandamano? Jibu rahisi ni kwamba wamefikia maendeleo kwa sababu ya kufanya kazi kwa bidii na kutumia muda ao vizuri kwa kuepuka au kuzuia matendo yote yanayoweza kuhatarisha Usalama na Amani.

Wahenga walisema kila zama na kitabu chake,hakika tumekuelewa Rais Dk. Magufuli kwa dhamira yako safi ya kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye ustawi wa kiuchumi.

Wananchi wote lazima wafurahie matokeo chanya ya rasilimali zilizopo hapa nchini, kwa dhamira safi ya kiongozi wetu ndoto hii imetimia kwa kuzingatia kuwa Watanzania hatuko tayari kufanya mambo ambayo yatahatarisha amani iliyopo.

Jambo la muhimu tuendelee kumwombea mtumishi wetu mwadilifu Rais Dk. Magufuli ili Mwenyezi Mungu ampe nguvu na ujasiri wa kuendelea kuwatumikia Watanzania.

Ni hakika kuwa Tanzania imeanza kujengewa msingi wa kuwa nchi ya asali na maziwa katika kipindi cha uongozi wa kiongozi wetu shupavu ambaye ameonyesha kuwa ametumwa na Mwenyezi Mungu kuwafikikisha Kanani Watanzania wote bila kujali vyama, dini wala makabila yao.

Katika historia Musa aliwavusha wana wa Israel katika BaharÌ ya Shamu, nasi tumeona juhudi za kiongozi wetu kutuvusha kuelekea nchi ya maziwa na asali, tunakupongeza Rais Dk. Magufuli, tunasema Hapa Kazi Tu.

Kila kona ya Tanzania, wananchi wengi wameonyesha kuwa hawana muda wa kushiriki maandamano na mambo yasiyo na tija kwa taifa na sasa ni wakati wa kujenga Tanzania mpya.

Ni lazima tuondokane na dhana ya uvivu na uzembe, kucheza karata, ‘pooltable’, kamari na mengine yanayofanana na hayo ili tutumie muda vizuri.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.