Nchi hatari zatajwa

Uhuru - - Habari - NEW YORK, Marekani

MALAWI, Kenya, na Afrika kusini zimetajwa kuwa ndio hatari zaidi kutembea kwa miguu na kuendesha baiskeli kwa mujibu wa utafiti wa Umoja wa Mataifa (UN, kuhusu ajali za barabarani.

Kati ya watu milioni 1.3 wanaofariki dunia kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, asilimia 49 ni watu wanaotembea, waendesha baiskeli na pikipiki, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) lilisema.

Malawi inaongozwa kwa vifo vinavyofikia asilimia 49 huku watembea kwa miguu wakiwa asilimia 14 hadi 17.

Idadi ya vifo hivyo nchini Kenya, imefikia asilimia 47 huku wanaotembea ikiwa ni asilimia 14.

Kwa upande wa Afrika kusini ni asilimia 50 huku vifo kwa wanaotembea kwa miguu ikifikia asilimia 3.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.