DC Arumeru aunda tume kuchunguza utoro kazini

Uhuru - - Habari -

MKUU wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti, ametuma timu ya uchunguzi katika vyuo vikuu vyote nchini, kwa ajili ya kupata idadi halisi ya watumishi wa wilaya hiyo walioko masomoni.

Mnyeti, alitoa kauli hiyo juzi, kutokana na idadi kubwa ya watumishi wa wilaya hiyo kuomba ruhusa za kwenda masomoni, lakini baadhi yao wanaonekana mitaani wakifanya shughuli binafsi, huku wakiendelea kupokea mishahara.

Alisema watumishi ambao watabainika kuwa hawapo masomoni na wanaendela kupata fedha za malipo ya masomo na mishahara, watakuwa wamejifukuzisha kazi wenyewe.

“Kuna idadi kubwa ya walimu, ambao wapo mitaani, lakini taarifa zinaonyesha kuwa wapo masomoni. Kama mkuu wa wilaya, sipo tayari kuona watumishi wakiidanganaya serikali, wote nitawafukuza kazi mara moja,”alisema.

Wakati huo huo, Mnyeti amewataka wakuu wote wa idara katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru, kumpa taarifa za madiwani wanaokwamisha miradi ya maendeleo katika kata zao.

Mnyeti alisema anazo taarifa za madiwani katika halmashauri hiyo, ambao wamekuwa wakikwamisha miradi ya maendeleo na kuwatisha wakuu hao wa idara, hali inayowafanya washindwe kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Aidha, aliwataka wakuu hao wa idara kutowaogopa madiwani kwa madai kuwa, watawafukuza kazi wakati wa vikao vya baraza la madiwani.

“Msiwaogope madiwani, hakuna mtumishi yeyote atakayefukuzwa kazi kwa ajili ya vitisho vya madiwani wanaokwamisha miradi ya maendeleo.

“Hao madiwani watakuwa wanawashwa na mimi kama mkuu wa wilaya, hivyo nitawakuna kikamilifu. Siwezi kuona wananchi wakikosa maendeleo kwa ajili ya vitisho vya madiwani,” alisema.

RAIS wa Zanzibar, Dk.Ali Mohammed Shein, akizungumza na viongozi wa Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto, Ikulu, mjini Unguja, jana (Picha na Ikulu).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.