Serikali yatoa tahadhari kwa halmashauri nchini

Uhuru - - Habari - NA ANITA BOMA, IRINGA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba, amezitaka halmashauri zote nchini kutoanzisha miradi ya umwagiliaji bila kupewa kibali kutoka kwa Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Mamlaka za Usimamizi wa Rasilimali za Maji kwenye mabonde husika.

Makamba, alitoa kauli hiyo juzi, baada ya kutembelea Mto Ruaha Mkuu, ambao ndiyo uti wa mgongo wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ni hifadhi kubwa kuliko zote nchini na Afrika Mashariki na kujionea maji yalivyokauka kwenye mto huo.

Alisema hali ya mto huo hairidhishi, hivyo ni lazima halmashauri zote kuzingatia agizo hilo ili kuunusuru mto huo na uharibifu wa mazingira unaotokana na miradi ya umwagiliaji inayoanzishwa kiholela.

ìKwa hiyo kama hayo hayafanyiki ni kosa na kama kuna mradi ambao umefanywa bila kupata kibali cha mamlaka ya bonde na NEMC, mradi huo unapaswa kusimama na kufungwa hadi tathmini ya athari ya mazingira ya mradi huo zitakapofanyika,îalisema Makamba

Alisema endapo kila halmashauri italizingatia hilo, watakuwa wamehifadhi mazingira kwa kiasi kikubwa kwa sababu tayari watakuwa wamepewa miongozo na usimamizi wa mazingira katika maeneo yao.

Makamba aliongeza sharti pekee la mwanafunzi kupata cheti cha kuhitimu elimu ya msingi kuwa ni kuhakikisha anaukabidhi uongozi wa shule mti wake, alioupanda siku alipokuwa akiingia shuleni hapo na kuutunza hadi anamaliza shule hiyo.

Sambamba na kuwataka wanafunzi wa shule za msingi kupanda mti mmoja, pia aliwataka wanafunzi wa shule za sekondari kupanda miche mitatu ya miti, ambayo wataitunza hadi watakapohitimu elimu yao ya sekondari ili nao washiriki kutunza mazingira kwa kupanda miti hiyo.

ìKutokana na hali hiyo ya uharibifu wa mazingira na uharibifu wa vyanzo vya maji, kuanzia Novemba 5 hadi Novemba 6, mwaka huu,

wizara tumewaita wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wenyeviti na mameya wote, kuja Arusha kwa ajili ya kuwapatia mafunzo na maelekezo mahsusi yanayoendana na uhifadhi wa mazingira, ikiwemo upandaji miti na utunzaji wa vyanzo vya mazingira,î alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, aliiomba serikali kuimarisha uwanja wa ndege wa Nduli, ulioko mjini hapa ili watalii wanaotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, watumie uwanja huo na kuwanufaisha wananchi wa mkoa huo.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa kazi ya usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa watumishi wa umma, mjini Dodoma, jana. Wa pili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah. Kairuki na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu ProjestRwegasira

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.