Wadau wa habari waongezewa muda

Uhuru - - Habari -

KAMATI ya Huduma za Jamii, imeongezea muda wa siku mbili kwa wadau wa habari ambapo badala ya siku saba wadau hao watatakiwa ndani ya siku tisa kutoa maoni yao mbele ya kamati hiyo kabla ya Novemba Mosi, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana katika ukumbi wa Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba, alisema wadau waliomba kuongezewa muda kwa madai kuwa waliopewa awali ulikuwa hautoshi.

ìBaada ya jana na kwa kweli wadau waliomba muda kwa sababu walisema walikuwa hawajaisoma sheria vizuri, kwa maana ya muswaada hivyo nimewaongezea siku mbili zaidi ambapo Jumamosi Oktoba 29, mwaka huu, tutakutana,îalisema Serukamba.

Alisema wakati wao wanaendelea kusoma muswada huo ili waweze kutoa maoni yao, kamati inaendelea na jukumu la kutunga sheria hiyo.

Alibainisha kuwa, juzi walianza kazi ya kupitia kifungu kwa kifungu hadi kufikia kifungu cha nne na wabunge wanatoa mawazo yao na mengine serikali imeyakubali na mpaka Jumanne watakuwa wamemaliza muswada wote.

ìHatutomaliza kabisa mpaka tupate maoni ya wadau na mawazo yao, mawazo ya wadau ambayo sisi tutakuwa tumeyafanyia kazi, yatakuwa yamejifuta moja kwa moja na yale ambayo tutaona yana maana katika kuboresha muswaada huo tutayaingiza.

ìNdio maana Oktoba Mosi na pili tutakutana na serikali ili tuweze kuingiza na maoni yaliyoletwa na wadau lakini kazi ya kutunga sheria hii tunaendelea nayo,îalisisitiza Serukamba.

Juzi, wadau hao wa habari walifika kwenye kamati hiyo kwa ajili ya kutoa maoni kabla ya muswada huo kupelekwa bungeni.

Hata hivyo, wadau hao waligomea kutoa maoni hayo kwa madai hawajapata muda wa kutosha kuusoma, hivyo kuomba waongezewa muda.

Muswada huo wa Sheria ya Huduma ya Habari ulisomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa Bunge uliopita, unatarajiwa kusomwa kwa mara ya pili na kupitishwa katika mkutano wa Novemba Mosi.

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akizindua kitabu kiitwacho ‘A-Concise Study of Contemporary Art’ kinachoeleza uhusiano na urafiki uliodumu kati ya Tanzania na Uswisi, Ikulu, Dar es Salaam, jna. Kushoto ni Balozi wa Uswisi nchini, Florence Tinguely. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.