Van Persie amkumbuka

Uhuru - - Matangazo -

Uturuki ISTANBUL,

STRAIKA wa Fenerbahce, Robin van Persie, amesema kuwa angeendelea kucheza Manchester United kama ingewa chini ya kocha Sir Alex Ferguson. Van Persie anayecheza timu ya taifa ya Uholanzi, alisajiliwa na Fenerbahce mwaka jana kutoka United. Mshambuliaji huyo aliamua kuondoka United kutokana na kushindwa kuonyesha kiwango bora chini ya kocha David Moyes na baadaye Louis van Gaal katika kikosi hicho. Amesisitiza kuwa huenda angekuwepo katika timu ya United hadi leo kama Ferguson angekuwa bado kocha wa timu hiyo kwani alikuwa chaguo lake. Alisema kuwa aliamua kwenda United akitokea Arsenal kwani aliamini Fergoson angedumu kwa muda mrefu katika kikosi hicho. Alisema kuwa mambo mengi kwenye mpira hubadilika mara kwa mara na hivyo mchezaji au kocha hawezi kuamua mwenyewe kwamba akae kwenye timu moja kwa muda gani. “Hadi sasa ningekuwa mchezaji wa Manchester United kama kocha Sir Alex Ferguson angekuwepo kwani nilikuwa mmoja wa wachezaji ambao ni chaguo lake,” alisema. Mdachi huyo alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka msimu wa mwaka 2012-13 akiwa katika kikosi cha United.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.