Bayern yamkuna Ancelotti

Uhuru - - Matangazo -

MUNICH, Ujerumani

KOCHA wa Bayern Munich, Carlo Ancelotti, ameonekana kukoshwa na matokeo aliyoyapata juzi kwenye mchezo wa makundi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya PSV. Katika mchezo huo, Thomas Muller na Joshua Kimmich walifunga bao moja kila mmoja kwenye kipindi cha kwanza kabla ya Luciano Narsingh kufunga bao pekee kwa PSV muda mchache kumalizika kipindi cha kwanza. Mchezaji Robert Lewandowski aliiongezea Munich bao la tatu ambapo Arjen Robben alimalizia karamu ya mabao kwa kufunga bao la nne dakika chache kabla ya kumalizika kwa mchezo huo. Kufuatia matokeo hayo, Munich inashika nafasi ya pili na kujihakikishia kusonga mbele kwenye michuano hiyo ambapo ina pointi sita huku vinara wa kundi D wakiwa Atletico Madrid ambao wana pointi tisa kwa kushinda mechi tatu. Kocha huyo amesema kuwa amefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na kikosi chake na hivyon anaamini timu hiyo itafika mbali msimu huu. “Tumecheza vizuri hicho nio ninachokitaka kwani wachezaji wamejituma na kuonyesha kuwa wana nia ya kufuika mbali msimu huu,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.