Stones achomoza Barcelona

Uhuru - - Matangazo -

BARCELONA, Hispania

BEKI wa kati wa Manchester City, John Stones, ametajwa kuwa mmoja wa wachezaji ambao wanaweza kufanya vizuri kama akitua Barcelona.

Mchezaji huyo juzi alionyesha kiwango bora pamoja na kuwa timu yake ilipoteza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa kwenye Uwanja wa Nou Camp.

Barcelona juzi iliutumia vyema uwanja wake wa nyumbani na kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 ambapo Lionel Messi alifunga hat trick na bao moja likiwekwa kimiani na mshambuliajin hatari Neymar.

Taarifa iluiyotoka kwenye mtandao wa klabu ya Barcelona, ilisema kuwa Stones alionyesha uwezo wa aina yake kwenye mchezo huo na kutwaja kuwa mmoja wa wachezaji wa England wanaoweza kumudu mikikimikiki kwenye kikosi cha Barcelona kama akipata nafasi.

Hata hivyo kabla ya kuanza kwa mchezo huo, kocha wa Man City Pep Guardiola, alisema kuwa ana imani na Stones kwani ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa anapokuwa uwanjani.

Taarifa hiyo ilisema kuwa kama uongozi ungefanikiwa kumsajili Stones msimu huu kikosi hicho kingeimarika zaidi ya kilivyo kwa sasa.

Barcelona ilitoa ofa nono kwa ajili yan kumsajili mchezaji huyo msimu huu na kwamba ingemlipa mshahara wa pauni 90,000 kwa wiki kama dili hilo lingekamilika.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.