Messi amjibu Guardiola

Uhuru - - Matangazo -

BARCELONA, Hispania

MSHAMBULIAJI wa timu ya Barcelona, Lionel Messi, juzi alimjibu bosi wake wa zamani, Pep Guardiola,baada ya kufunga mabao ‘matatu’ hat trick katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa Uwanja wa Nou Camp.

Barcelona iliikaribisha Man City katika mchezo huo uliokuwa na upinzani mkali na kushinda kwa mabao 4-0.

Messi alipiga hat trick ya 37 kwenye kikosi hicho huku akitoa pasi ya mwisho ya bao lililofungwa na Neymar.

Katika mchezo huo kipa wa Man City, a Claudio Bravo, alitolewa kwa kadi nyekundu na kusababisha timu yake kucheza pungufu kwa muda.

Guardiola (pichani), alisema kuwa mchezo huo haukuwa rahisi kwake kwani wachezaji wake walipata nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia.

“Mchezo haukuwa rahisi kwani tulicheza pungufu kwa muda hadi pale tulipokuwa sawa, lakini straika ya Barcelona ninaijua na ukiipa nafasi inazitumia vilivyo.

“Kila mtu anapenda kuona tunapata matokeo mazuri kipa alituwekea wakati mgumu baada ya kuadhibiwa na kadi nyekundu kutokana na kurudia makosa yaleyale,” alisema Guardiola.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.