Kipa nguli afariki England

Uhuru - - Matangazo -

LONDON, England

KLABU ya Leeds United, imepata pigo baada ya kuondokewa na kipa wake wa zamani Gary Sprake.

Leeds juzi ilitangaza kuondokewa na kipa huyo wa zamani ambaye alikuwa akijulikana kwa jina la utani Careless Hands’ baada ya kuugua kwa muda.

Sprake ambaye alizaliwa mwaka 1945 amefariki juzi akiwa na umri wa miaka 71 ambapo awali alishawahi kuichezea timu ya taifa ya Wales.

Kipa huyo ameichezea Leeds zaidi ya mechi 500 enzi za uhai wake katika michuano mbalimbali Ulaya kwa kipindi cha miaka 11.

Sprake aliwahi kuwa mmoja wa makipa ghali zaidi ulimwenguni pale aliposaini mkataba mpya na Birmingham City kwa dau la pauni 100,000.

Enzi za uhai wake alishawahi kushinda mataji mbalimbali kwenye timu ya Leeds kama vile Fairs Cup na kombe la Ligi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.