Cheka apewa Dulla Mbabe

Uhuru - - Michezo - NA AMINA ATHUMANI

PROMOTA maarufu wa ngumi za kulipwa nchini Kaike Siraji ameamua kumaliza ubishi wa mabondia wababe nchini Fancis Cheka na Abdallah Pazi ‘Dulla mbabe.

Cheka na Dula Mbabe watavaana Desemba 26, mwaka huu katika ukumbi wa Jamhuri mjini Morogoro.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaike alisema pambano hilo la kufunga mwaka litakuwa ni la raundi 10 ambalo litachezwa na wababe hao wanaotambiana kila kukicha.

Kaike alisema Dula Mbabe na Cheka ni mabondia wenye rekodi nzuri katika mchezo huo ndani na nje ya nchi hivyo kukutana kwao itaonesha dhahiri nani mwamba kwa mwenzake,

Alisema pambano hilo litatanguliwa na mapambano makali ya utangulizi likiwemo la ubingwa wa Dunia wa UBO kati ya Chimwemwe Chiota dhidi ya Thomas Mashali ‘Simba Asiyefugika’.

Alisema ubingwa mwingine utakuwa ni wa UBO Afrika utakaogombewa na Twaha Kiduku dhidi ya Chazama ambalo pia litakuwa nipambano kubwa.

Mapambano mengine yatakuwa kati ya Mohamed Matumla dhidi ya Deo Samwel na Man Chugga atapigana na Kudura Tamimu.

“Maandalizi ya mapambano yote yameshaanza na mabondia wanaendelea kujifua kwa ajili ya mapambano hayo, ni waahidi watanzania na wana Morogoro itakuwa ni burudani kubwa na ya kusisimua katika mchezo huu,”alisema Kaike.

FANCIS Cheka

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.