Ngassa apigwa ‘stop’

Uhuru - - Michezo - NA ATHANAS KAZIGE, MWANZA

KOCHA Msaidizi wa Toto Africans, Khalfan Ngassa, amesema kuwa alishindwa kukaa katika benchi la timu hiyo katika mchezo dhidi ya Yanga kutokana na kukosa kibali.

Akizungumza juzi jijini hapa, alisema alishindwa kukaa katika benchi la Toto kutokana na kukosa kibali cha kufanya kazi.

Kocha huyo kwa sasa ndio ana kaimu nafasi ya kocha mkuu baada ya kujiuzulu aliyekuwa kocha wa timu hiyo Rogatian Kaijage.

Kaijage, aliamua kuachana na timu hiyo baada ya kushinikizwa kuondoka na wanachama, wapenzi na mashabiki wa soka mkoani kutokana na timu hiyo kufungwa na Mbao FC.

“Sina kibali, ndio maana nilikuwa jukwaani, lakini najua viongozi wangu wanafuatilia kibali hicho kutoka Bodi ya Ligi Kuu na Shirikisho la Soka la Soka Tanzania TFF,”alisema Ngasa.

Katika mchezo huo, Toto Africans ilifungwa mabao 2-0 yaliwekwa wavuni na wachezaji, Simon Msuva na Obrey Chirwa.

Akizungumzia mwenendo wa timu yake, Ngasa alisema wataendelea kufanyia kazi kasoro zilizotokea na kusababisha timu hiyo kufungwa na Yanga kwenye uwanja wake wa CCM Kirumba.

“Mimi ndio mechi ya pili kuiongoza Toto ingawa nilikuwa jukwani, tuna programu nataka kuifanya ili tufanye vizuri,”alisema Ngassa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.