Filbert Bayi anogewa TOC

Uhuru - - Michezo - NA AMINA ATHUMANI

KATIBU mkuu wa Kamati ya OlimpikiTanzania (TOC) anayemaliza muda wake, Filbert Bayi, amesema umri unamruhusu kugombea tena uongozi katika kamati hiyo.

Kauli ya Bayi inatokana na baadhi ya wadau wa soka, kurusha vijembe kuwa uongozi wa wake umeongoza kamati hiyo kwa muda mrefu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Bayi alisema kwa mujibu wa sheria za Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC), mwisho wa ukomo wa mgombea ni miaka 70.

Bayi alisema kwa umri alionao sasa unampa nafasi ya kugombea tena kwenye kamati hiyo kama atataka kufanya hivyo.

Alisema hata hivyo anaamini hatafikia umri wa miaka 70 kwa kuwa kabla ya kufika huko ataacha kugombea na kuwapa nafasi wengine.

Kuhusu uchaguzi wa mwaka huu utakaofanyika Desemba 10, mwaka huu mjini Dodoma, Bayi alisema atatanga kama atagombea au hatogombea muda utakapofika.

Fomu za kuwania uongozi wa kamati hiyo zitaanza kutolewa Oktoba 25 mwaka huu.

Katika uongozi unaomaliza muda wake Rais anaekalia kiti hicho kwa sasa ni Gulam Rashid.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.