Uganda kundi la kifo Afrika

Uhuru - - Michezo - LIBREVILLE, Gabon

TIMU ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ imepangwa kundi la kifo katika michuano ya Kombe la Afrika.

Uganda ndio timu pekee kutoka Afrika Mashariki na Kati inayoshiriki Kombe la Afrika (AFCON), nchini Gabon, mwakani.

Uganda ilifuzu hatua ya makundi, baada ya kumaliza kundi lao katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 10.

Uganda imepangwa kundi gumu la D na timu za Ghana, Mali na Mirsi ambalo linaweza kuwa mwiba kwa timu hiyo inayonolewa na Mserbia Sredojevic Milutin ‘Micho’.

Micho, aliwahi kuifundisha Yanga na anatajwa kuwa mmoja wa makocha bora Afrika mwenye uzoefu wa kutosha.

Ratiba iliyopangwa juzi usiku inaonyesha kuwa Kundi A litakuwa na wenyeji Gabon, Burkina Faso, Cameroon na Gueine Bissau.

Kundi B linaundwa na timu za Algeria, Tunisia, Senegal na Zimbabwe.

Kundi C litazikutanisha timu za Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Morocco na Togo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.