Jubilee yagawanyika kuhusu marekebisho ya Katiba

Taifa Leo - - Front Page - Ripoti ya Patrick Lang’at, Florah Koech na Steve Njuguna

Na WANDISHI WETU

PENDEKEZO la kinara wa ODM Raila Odinga kutaka Katiba ifanyiwe mabadiliko limegawanya chama cha Jubilee.

Kile kimejitokeza ni kuwa wabunge wa uliokuwa mrengo wa TNA wanataka mabadiliko huku wa URP wakipinga.

Miongoni mwa waliojitokeza kuunga mkono ni Mbunge Maalum Maina Kamanda, Moses Kuria (Gatundu Kusini), Michael Muchira (Ol-joro Orok, Kinuthia Gachobe (Subukia), Kimani Kuria (Molo), Bi Faith Gitau (Mwakilishi wa Kike wa Nyandarua), Patrick Mariru (Laikipia Magharibi), Patrick Munene (Chuka-igamba-ng’ombe) na Bw Peter Kimari (Mathioya).

Wabunge hao wanasema kubadilisha Katiba kutasaidia kupunguza mzigo wa kulipa ushuru wa juu.

Lakini Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen amepuuzilia mbali wito wa kuandaa kura ya maamuzi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.