KNUT na TSC kuanza mashauriano leo kuhusu malalamishi ya walimu

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Ouma Wanzala

CHAMA cha Kitaifa cha Walimu (KNUT) leo kitaanza mkutano wa siku tano na mwajiri wao kujadili masuala tata ambayo nusura yasababishe mgomo mwanzoni mwa muhula huu.

Miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa ni kuhusu kupandisha walimu vyeo, pingamizi yao kuhusu utathmini wa utendakazi na uhamisho wa walimu miongoni mwa mengine.

Mkutano huo utakaofanyika Naivasha na kuhudhuriwa na wanachama wanane uliandaliwa wakati walimu walitishia kufanya mgomo. Inatarajiwa utasaidia kupata muafaka kati ya KNUT na Tume ya Kuajiri Walimu (TSC).

Katibu Mkuu wa KNUT, Bw Wilson Sossion, jana alisema chama chake kina matumaini kwamba TSC itatatua masuala ambayo walimu wamekuwa wakilalamikia.

"Tunataka mahitaji yetu yatimizwe na TSC ili tuwe na mazingara bora ya elimu nchini," akasema Bw Sossion.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.