Gavana afuta kazi mawaziri baada ya kuwarudisha kazini

Taifa Leo - - Kurunzi Ya Pwani - Na Kalume Kazungu

GAVANA wa Kaunti ya Lamu, Fahim Twaha aliwafuta kazi upya mawaziri wake wawili saa chache baada ya kuwarejesha kazini. Wawili hao, Bw Raphael Munyua Ndung’u (Afya na Mazingira) na Bi Florence Wairimu Ndung’u (Kilimo na Maji) walikuwa wamefutwa kazi miezi sita iliyopita lakini wakarudishwa kazini Alhamisi kufuatia amri ya mahakama.

Aidha kurejeshwa kwao kazini kulikuwa kwa muda tu kwani baadaye Bw Twaha aliwafuta kazi tena.

“Mawaziri hao awali walikuwa wamepigwa kalamu lakini walipoenda kortini, mahakama ilidai mpangilio uliotumika kuwafuta kazi haukufaa. Gavana alitii amri ya korti na akawarudisha mawaziri hao kazini. Sasa ameafikia kuwafuta kazi kwa kufuata mpangilio ufaao,” akasema mmoja wa maafisa wakuu wa serikali ya kaunti ya Lamu aliyeomba asitajwe.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.