Kaunti yashindwa kuzuia ujenzi wa chuo cha Mombasa

Taifa Leo - - Kurunzi Ya Pwani - Na Philip Muyanga

UJENZI wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Mombasa utaendelea sasa baada ya serikali ya kaunti kupoteza rufaa dhidi ya uamuzi uliofutilia agizo lake la kusimamisha ujenzi wa chuo hicho.

Uamuzi huo ni pigo kubwa kwa serikali ya kaunti ya Mombasa iliyokuwa imekata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama kuu uliofutilia mbali notisi iliyokuwa imeipatia African University Trust of Kenya (AUTK) ambao wanajenga chuo hicho, kusimamisha ujenzi.

Majaji wa mahakama ya rufaa Alnashir Visram, Wanjiru Karanja na Martha Koome walisema kwa kuwa serikali ya kaunti ilikuwa imetoa ruhusa ya ujenzi wa chuo hicho mwanzo, ilimaanisha ya kuwa masharti yote yalifuatwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.