‘Mafisi’ mtaani waachwa na kiu windo kuwaponyoka

Taifa Leo - - Dondoo! - Na MWANDISHI WETU

Mafisi wa mitaani waliachwa na kiu pale mama mmoja alipoanika siri zake za chumbani bila kujua kabla ya kugundua kosa lake na kuhepa.

Kwa mujibu wa mdokezi wetu, siku ya kituko hiki, mama huyo alifika mjini kufanya shughuli zake. Hata hivyo, baada ya kutoka katika duka moja kwenye barabara hii, alianza kuropoka hadi akafichua kwamba hakuwa amefanya tendo la ndoa kwa kipindi cha mwaka mzima.

“Aisee! Natamani sana kuwa na mwanamume. Nina kiu kali ya tendo la ndoa. Ni muda mrefu…siamini ni mwaka mmoja mzima sijafanya mapenzi. Natamani mwanamume,” mama huyo alisikika akisema akiwasiliana kwa simu.

Hata hivyo, sauti yake haikuwa ya kimoyomoyo na ilitosha kufika maskioni mwa mafisi waliokuwa karibu na hawakusita kuanza kumtupia macho ya tamaa wakitaka kumshughulikia.

Mama alipogundua sauti yake iliamsha mafisi kutoka usingizini, alibadili wimbo. “Tafadhali sahau nilichosema. Niko sawa. Sitaki mwanamume. Niko sawa kabisa,” alisema jombi mmoja alipomrushia chambo pap.

Inasemekana baadhi ya makalameni walimwandama wakiahidi kumhudumia akate kiu lakini alikwepa kila ndoano kabla ya kutimka mbio.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.