Adai Mungu alimrushia 1,000 akienda kanisani

Taifa Leo - - Dondoo! - Na STEPHEN DIK

MUUMINI wa kanisa moja mjini hapa alishangaza kwa ushuhuda wake kwamba Mungu alimrushia Sh1000 akienda kanisani. Jamaa alimsifu Mungu na kushukuru akisema aliweza kuokota pesa alipokuwa na shida. Alizidi kutoa ushuhuda akisema pesa alizookota njiani ni Mungu aliyemrushia na hazikuangushwa na mwanadamu.

Inasemekana jamaa alitoa sadaka ya Sh2000 kama shukrani kwa Mungu. Jamaa alichukua muda mrefu akishukuru Mungu kwa zawadi hiyo hadi waumini wakaanza kulalamika.

Pasta alimpokonya kipaza sauti na kumaliza ibada kwa sababu ibada ilikuwa imechelewa kumalizika.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.