Sossion akomeshe vitisho

Taifa Leo - - Barua -

KATIBU Mkuu wa Chama cha Kitaifa cha Walimu (KNUT) Wilson Sossion, kwa mara nyingine ametishia huenda walimu wakafanya mgomo katika majuma mawili yajayo ikiwa matakwa yao hayatimizwa na serikali.

Kamwe hatuwezi kuwa na shida kuhusu elimu kwa watoto wetu mara kwa mara. Tusisahau tunangoja mitihani ya kitaifa itakayofanywa hivi karibuni.

Bw Sossion anastahili kuendelea na siasa zake bila kuhusisha elimu yetu kwani anatatiza wanafunzi wetu kimasomo na kuwatia hofu wanaposubiri mitihani.

KIM NJUGUNA, Gachoka, Kiambu

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.