Hima walimu wa Mombasa

Taifa Leo - - Barua -

KAUNTI ya Mombasa imetajwa sana kwa kuandikisha matokeo duni katika mitihani ya kitaifa ya KCPE na KCSE.

Kuna sababu kadhaa ambazo husemekana kuwa chanzo cha hali hii, mojawapo ikiwa ni kutokamilisha silabasi.

Ikiwa zimesalia siku chache kabla mitihani ya kitaifa kuanza, walimu wanafaa kufanya hima kukamilisha silabasi ili wanafunzi wapate muda mwafaka wa kufanya marudio.

Hili likifanikishwa huenda likasaidia pakubwa kuimarisha kiwango cha elimu Mombasa na tutashuhudia matokeo bora kutoka kwa wanafunzi wetu.

EDWIN FUMBA, Kenya Coast National Polytechnic

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.