Wabunge wetu wastaarabike

Taifa Leo - - Barua -

JUMA lililopita, hali ya mshikemshike ilishuhudiwa bungeni baada ya wabunge kuamua kuanika sarakasi zao kwa mamilioni ya Wakenya wakati wa kupitisha mswada wa fedha kuhusu utozaji ushuru.

Badala ya kukaa na kujadili masuala muhimu ya ujenzi wa taifa, wabunge hawa waliyafanya mambo yao kienyeji wakiwa wamesimama huku kila mmoja wao akiwa anazungumza ovyo bila ya utaratibu wowote.

Ili kusikilizwa, silaha tosha huwa ni utulivu na utu uzima, bali si tabia ya kupayuka na kuropoka ovyo na hatimaye kulaumu wengine kila wakati.

Maoni yangu ni kwamba, wabunge wastaarabike hasa kwa jinsi wanavyofanya mambo yao bungeni kwani ndio wawakilishi wa raia bungeni.

WAFULA W. ANTHONY, Shule ya Upili ya Teremi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.