Wachezaji walivyobwaga TP Mazembe katika kivumbi cha Klabu Bingwa Afrika

Taifa Leo - - Dimba -

MABINGWA wa zamani wa taji la Klabu Bingwa barani Afrika (CAF Champions League), TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya

Congo, kwa masikitiko makubwa waliondolewa katika hatua ya robo-fainali ya kipute hicho mwaka huu.

Hatua hii ilikuja baada ya mechi ya hivi karibuni iliyowakutanisha na

Primero de Agosto ya Angola, ambayo ilifuzu kwa nusu-fainali kwa faida ya bao la ugenini.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Luanda, TP Mazembe hawakufungana na wenyeji wao, lakini mambo yalikuwa si mazuri sana baada ya kuambulia sare ya 1-1 nyumbani na kwa mujibu wa kanuni za CAF, mgeni alinufaika na bao hilo muhimu.

Safari ya TP Mazembe msimu huu haikuwa rahisi. Ilikuwa katika kundi moja na ES Setif ya Algeria, Difaa El Jadida ya Morocco na MC Alger ya Algeria. Matumaini yalianza kuonekana baada ya Mazembe kushinda mechi tatu kati ya sita walizocheza na kutoka sare katika michuano mingine mitatu na kutofungwa katika mechi zote sita ilizocheza.

TP Mazembe ilianza vyema nyumbani kwa kuishinda ES Setif kwa mabao 4-1. Katika mechi ya pili, ilipata matokeo mazuri baada ya kuishinda Difaa El Jadida ya Morocco 2-0. Katika matokeo mengine, TP Mazembe walitoka 1-0 na MC Alger nyumbani kabla ya kusajili sare ya 1-1 ugenini. Baadaye waliambulia sare ya 1-1 dhidi ya ES Setif na kusajili matokeo sawa na hayo dhidi ya Difaa El Jadida.

Nimetoa matokeo hayo ili uelewe kwa urahisi namna safari ya klabu hii ilivyokuwa na ujaribu kujiuliza na kujijibu ni kwanini TP Mazembe iliangukia mlangoni.

Tunajadili klabu hii kwa sababu ni timu kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambayo ina wafuasi wengi, kutokana na uwezo wake wa kucheza soka na kupata matokeo mazuri. Hakuna anayeweza kusahau fainali ya mwaka 2010 ya kuwania ubingwa wa klabu bingwa duniani, ilipocheza na Inter Milan ya Italia na kwa bahati mbaya kufungwa katika uwanja wa Zayed mjini Abu Dhabi.

Nakumbuka baadhi ya wachezaji maarufu waliokuwa katika mechi hiyo ni pamoja na kipa Robert Kidiaba, anayekumbukwa sana kwa namna anavyoshangilia goli linapofungwa bila kumsahau nahodha Pamphile Mihayo Kazembe ambaye kwa sasa ndiye kocha wa klabu hiyo yenye makao yake jijini Lubumbashi.

Hakuna asiyefahamu kuwa, klabu hii imeshinda taji hili mara tano, mara ya mwisho ikiwa ni 2010. Imewahi pia kushinda taji hili mnamo 1967, 1968, 2009, 2010 na 2015.

Baada ya kutoa tathmini kuhusu klabu hii, nisema tu kuwa, TP Mazembe iliondolewa katika michuano hii baada ya wachezaji kukosa utulivu na umakini uwanjani katika mechi zao.

Nasema hivi kwa sababu klabu hii ilikuwa na uwezo mkubwa wa kushinda mechi ya mwisho kwa namna mazingira yalivyokuwa.

Kwanza mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa Stade du TP Mazembe mjini Lubumbashi. Mambo yalikuwa mabaya zaidi baada ya wachezaji wawili kukosa nafasi adhimu za kupata mabao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.