Mashabiki wataka Mou afurushwe Old Trafford

Taifa Leo - - Gumzo La Spoti -

Baada ya klabu yao kubanduliwa na Derby County katika michuano ya Carabao Cup, mashabiki sugu wa Man-united sasa hawamtaki tena kocha Jose Mourinho. Kuna uwezekano mkubwa wa Zinedine Zidane kupokezwa jukumu la kuwanoa Man-united iwapo klabu hiyo itaendelea kuwapa machungu mashabiki hao. Majuzi, Zidane alionekana na mkewe jijini London, Uingereza. Wapigaji picha walimpata kocha huyo wa zamani wa Real karibu na uwanja wa Old Trafford lakini hawakufanikiwa kumhoji. Wengi wa mashabiki wa Man-united wanamtaka Zidane atue Trafford.

Picha/afp

Kocha Jose Mourinho wa Manchester United.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.