Pogba kupigwa mnada, uhusiano wake na Mourinho umeingia mdudu

Taifa Leo - - Gumzo La Spoti -

Baada ya kuchoshwa na kiungo Paul Pogba, kocha Jose Mourinho amesema kwamba atalazimika kumuuza nyota huyo mzawa wa Ufaransa. Ripoti za vyombo vya habari nchini Uingereza zimesema kwamba thamani ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 sasa imefikia Sh30 bilioni.

Pogba anatarajiwa kuondoka uwanjani Old Trafford mwezi Januari 2019, mwaka ujao baada ya uhusiano wake na Mourinho kuporomoka kabisa. Majuzi, kocha huyo mzawa wa Ureno alimpokonya staa huyo majukumu ya unaodha baada ya Manchester United kutoka sare ya 1-1 na Wolves. Mourinho alimfokea nyota huyo akidai ndiye aliyefanya makossa ambayo yaliwazawidia Wolves nafasi ya kufunga bao la kusawazisha.

Picha/afp

Pogba aondoka ugani shingo upande baada ya kutolewa dhidi ya Wolves ugani Old Trafford mnamo Septemba 22, 2018.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.