Pigo kwa Buhari baada ya waziri mwingine kutangaza kujiuzulu

Taifa Leo - - Habari Za Afrika Na Dunia -

WAZIRI wa masuala ya wanawake wa Nigeria Jumamosi aliwasilisha barua ya kujiuzulu kwa Rais Muhammadu Buhari katika pigo la hivi punde kwa chama chake kabla ya uchaguzi wa urais unaotarajiwa Februari.

Aisha Alhassan ni waziri wa pili kujiuzulu mwezi huu baada ya Kemi Adeosun aliyekuwa waziri wa Fedha.

" Leo, Septemba 29, ninataka kuwasilisha kwa rais uamuzi wangu wa kijiuzulu kama Waziri wa Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria na kama mwanachama wa chama cha All Progressive Congress (APC)," Alhassan aliandika kwenye Twitter.

Kwenye barua aliyomtumia Buhari Alhassan alisema alijiuzulu kutoka chama tawala kwa sababu alizuiwa kugombea kiti cha ugavana cha jimbo la Taraba lililoko Mashariki mwa nchi hiyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.