Waasi waua wanajeshi na wanawake DRC

Taifa Leo - - Habari Za Afrika Na Dunia -

Wanajeshi wawili na wanawake wawili waliuawa kwenye mashambilizi katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, afisa wa serikali alisema Jumamosi.

Waasi wa Kihutu kutoka Rwanda walivamia kambi ya kijeshi eneo la Mutabo na kuua wanajeshi wa Congo, msemaji wa jeshi katika eneo hilo Meja Guillaume Djike aliambia AFP.

Kundi la Allied Democratic Forces (ADF), lililotimuliwa Uganda ambapo liliua watu wengi tangu 2014 lililaumiwa kwa kuvamia kijiji cha Mukoko ambapo wanawake wawili waliuawa na watu kutekwa, afisa mmoja alisema.

Walioshuhudia walisema kundi la watu walikuwa wamekusanyika katika mji wa Beni mili ya wanawake hao ilipoletwa lakini polisi waliwatawanya kuepuka maandamano.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.