Waliojaribu kuua Waziri Mkuu sasa kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi

Taifa Leo - - Habari Za Afrika Na Dunia - Na MASHIRIKA

watano wanaokabiliwa na mashtaka ya kujaribu kumuua waziri mkuu sasa watashtakiwa kwa makosa ya ugaidi.

Mwendesha mashtaka mkuu wa Ethiopia aliwasilisha mashtaka hayo mapya dhidi ya watu hao waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka kufuatia shambulio katika mkutano mkubwa jijini Addis Ababa mnamo Juni.

Mashtaka yaliyowasilishwa Ijumaa yanasema kwamba watano hao walichukua hatua hiyo kwa sababu waziri mkuu Abiy Ahmed sio maarufu miongoni mwa jamii ya Oromo ambayo ni kubwa katika nchi hiyo na walitaka kutambuliwa kwa chama kilichopigwa marufuku cha Oromo Liberation Front.

Viongozi wa chama hicho walirejea Ethiopia baada ya serikali ya Abiy kualika makundi yote yaliyokuwa uhamishoni kushiriki siasa.

Watu wawili waliokufa na bomu lilipotupwa katika jukwaa Abiy alipokuwa akiwapungia mkono watu. Wengine zaidi ya 150 walijeruhiwa.

Shirika la habari la Ethiopia, Fana, liliripoti kuwa baadhi ya waliohusika hawajakamatwa.

Abiy ndiye waziri mkuu wa kwanza kutoka jamii ya Oromo na taharuki katika nchi hiyo ni tisho kwa mageuzi aliyoanzisha.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.