Maelfu ya wapinzani waandamana dhidi ya Rais Roch Kabaore

Taifa Leo - - Habari Za Afrika Na Dunia -

ya wafuasi wa upinzani Jumamosi waliandamana katika barabara za jiji kuu la Burkinabe, Ouagadougou katika maandamano ya kwanza makubwa dhidi ya Rais Roch Marc Christian Kabaore.

"Tunakataa ukosefu wa usalama, ugaidi, tunakataa upinzani na ukosefu wa ajira,” waandamanaji hao waliimba katika maandamano ya kwanza yaliyoitishwa na upinzani baada ya Kabaore kushinda uchaguzi wa Novemba 2015.

“Tuko hapa kwa sababu nchi imo hatarini,” alisema kiongozi wa upinzani Zephyrin Diabre.

Burkina Faso, inayopakana na Mali naniger, imekubwa na mashambulizi mabaya zaidi ya kigaidi tangu 2015 hasa maeneo ya Kaskazini na Mashariki ambako watu zaidi ya 60 wameuawa.

Wanajeshi wanane waliuawa kwenye mlipuko kaskazini mwa Burkina Faso Jumatano wiki jana.

Mnamo Jumapili wachimba migodi watatu, walitekwa na watu waliokuwa na silaha kati ya Djibo na migodi iliyoko eneo hilo.

Saa chache baadaye, polisi watatu waliotumwa kuwaokoa waliuawa kwenye makabiliano na watu waliokuwa na silaha eneo la Tongomael.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.