Nyota

Taifa Leo - - Fumbo & Falaki - Na Sheikh Khabib

KONDOO

Machi 21 – Aprili 20: Mambo ya kisheria yaliyokwama yanaweza kuluhishwa kwa wakati huu. Anza kufanya hivyo sasa kwa sababu huna wakati mrefu wa kutimiza kila kitu. Naona mpinzani wako akijiandaa kwa makabiliano.

NG'OMBE

Aprili 21 – Mei 20: Ni siku njema kwa kila jitihada za kubadilisha maisha yako ambazo ulikuwa nazo zikakuvunja moyo. Utawapendeza watu wengine na watasikiliza kila unalowaambia.

MAPACHA

Mei 21 – Juni 21: Itakuwa siku ya furaha kwako na familia yako. Nenda kawasilishe ombi la kibali ulichonyimwa tena. Kaa katika mipango yako na utafurahia siku hii. Usiombe mtu yeyote kitu leo.

KAA

Juni 22 – Julai 22: Mipango yako yote itafaulu. Weka watu wa familia yako mbele, lakini chunga wasikuvurugie mipango yako ya mahaba. Jiepushe na mambo mengine yaliyo kando na mipango yako wakatayokuletea.

SIMBA

Julai 23 – Agosti 22: Vizingiti vyote vimeondolewa na nyota yako inaangaza nuru ya ajabu. Chaguo ni lako ikiwa utafanikiwa au la. Wacha mvutano na jirani yako uone mambo yakibadilika. Mitihani ya maisha imepungua.

MASHUKE

Agosti 23 – Septemba 23: Utakutana na mgeni afanye urafiki nawe. Hii ni fursa nadra sana katika maisha yako na ukiitumia vyema itakufaa kwa siku nyingi. Jihadhari usiseme uongo. Mgeni ni baraka.

MIZANI

Septemba 24 - Oktoba 23: Elekeza akili zako katika masuala ya watu wako ambayo unadhani yanahitaji kuangaliwa vyema.punguza starehe ninazoona zimekulemea. Usitoe pesa zozote benki ikiwa huna mipango maalumu.

NGE

Oktoba 24 – Novemba 22:Kwa mara ya kwanza katika muda wa miezi mitatu matatizo ya afya yataisha. Toka ukalipe ahadi ambayo hukutimiza kabla ya mambo kuharibika. Naona kuna masaibu meng yanayokuzunguka kutokana na deni hii.

MISHALE

Novemba 23 – Desemba 21: Nenda ukakutane na mkubwa aliyekutimua kazi umweleze ukweli wa mambo. Usiseme uongo na uombe msamaha. Naona akikukaribisha na kukusikiliza. Huu ni wakati wa kulainisha mambo.

MBUZI

Desemba 22 – Januari 20: Usijihusishe na shughuli za kupoteza muda. Miradi yako imekwama kwa sababu hii. Huu ni wakati mzuri wa kufanya uamuzi wa busara wa pesa. Weka mpango mzuri ili ufurahie maisha siku zijazo.

NDOO

Januari 21 – Februari 19: Raha uliyonayo ni ya muda tu.unashauriwa ujipange vyema mapema, ujiandalie tukio lolote la kimaisha ambalo bila shaka litakupata. Jumuika na watu walio na maono sawa na yako.

SAMAKI

Februari 20 – Machi 20: Ni wakati wa kugutuka uache kuwaamini watu wa jinsia kinyume na yako. Nyota yako inasema umepoteza muda na mali nyingi ukiwasaidia ingawa baadhi ni walaghai. Ni wakati mzuri wa kutazama mbele na kuona maisha ya baadaye yatakavyokuwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.