Zion Winners, Cheza Sports nyembe gozini

Taifa Leo - - Spoti - Na Patrick Kilavuka

ZION Winners walipata ushindi mwembamba wa 2-1 dhidi ya Pelico katika mchuano wa ligi ya FKF Kaunti Tawi Nairobi West uwanjani Kihumbuini, wikendi. Brian Obanda aliona lango dakika ya 35 kabla ya Tom Ombagi kufyatua fataki dakika ya 40 na kufanya mambo kuwa 2-0 wakati wa mapumziko. Wapinzani walipunguza mwanya wa magoli dakika ya 48 kupitia kwa Alex Odhiambo. Cheza Sports iliilima KSG 3-1 katika mechi nyingine ya ligi hii.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.