Zimlatt yaramba vipusa wa Joho

Taifa Leo - - Spoti - Na Charles Ongadi

LIGI ya soka ya kinadada Mombasa ilinoga wikendi iliyopita, huku mechi mbili zikipigwa katika uwanja wa Shimo la Tewa Borstal. Shule ya Upili ya Zimlatt ililimea Hassan Joho Girls kwa mabao 2-1. Mwanasiti Ibrahim aliweka Joho Girls kifua mbele dakika ya 18, lakini Halima Mohammed akasawazisha dakika ya 42. Zimlatt iliendeleza harakati zake za kusaka bao la ushindi na kufanikiwa dakika ya 78 kupitia mchezaji Rose Mutavi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.