Makongeni ngoma ya MYSA FC ligini

Taifa Leo - - Spoti - Na Lawrence Ongaro

MYSA FC iliipepeta Makongeni Youth kwa mabao 3-1 katika Ligi ya Kaunti Ndogo ya Thika uwanjani St Patrick's, Jumamosi. Vijana wa MYSA walipata bao la kwanza dakika ya 28 kupitia kwa Sammy Maina. David Waweru aliongeza la pili dakika ya 37. Makongeni ilirejesha goli moja dakika ya 42 kupitia mchezaji Benard Kimani. Bao la ushindi la MYSA lilifumwa kimiani na George Kamau dakika ya 70.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.