Kocha: Wavamizi wangu ovyo langoni

Taifa Leo - - Spoti - Na Titus Maero

KOCHA Fidelis Kimanzi wa Wazalendo amelaumu utepetevu miongoni mwa wachezaji wake baada ya timu yake kulimwa 2-1 na Western Jaguars kwenye Ligi Kuu ya Magongo ya Wanaume, Jumamosi. Kimanzi alikashifu hasa wavamizi wake Sylvester Samo, Stephen

Liyai na Oliver Cheloti kwa kupoteza nafasi nyingi nzuri. Kimanzi, ambaye aliwahi kunoa timu ya taifa ya wanawake, alisema atawafanyisha washambuliaji wake mazoezi makali ya kukabiliana na wapinzani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.