Neymar achochea waajiri wake PSG kupaa zaidi Ligue 1

Taifa Leo - - Spoti -

NYOTA Neymar Jr alifunga magoli mawili na kuchochea Paris Saint-germain (PSG) kuendeleza rekodi ya kutoshindwa hadi kufikia sasa msimu huu kwa kuwapiga Nice 3-0 katika Ligue 1. Fowadi huyo mzawa wa Brazil aliwaweka waajiri wake kifua mbele kunako dakika ya 22 kabla ya kuelekeza fataki nyingine langoni pa wapinzani waliomaliza mchuano huo wakiwa na wachezaji 10 uwanjani. Christopher Nkuku alijifunga mwanzoni mwa kipindi cha pili kabla ya Neymar kukizamisha kabisa chombo cha wenyeji wao katika dakika ya 92. Kiungo wa Nice Wylan Cyprien alionyeshwa kadi nyekundu katika kipindi cha pili baada ya kulishwa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.