Simanzi aliyetarajia kuingia Kidato cha Kwanza 2019 kufa barabarani

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Magdalene Wanja

MSICHANA wa miaka 14 aligongwa na gari ndogo na kufariki dunia papo hapo na nduguze kupata majeraha mabaya wakati wa ajali Jumatano jioni.

Ajali hiyo ilitokea eneo la Sachangwan katika barabara lenye shughuli nyingi ya Nakuru - Eldoret.

Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, gari hilo lililokuwa likielekea upande wa Eldoret, lilikuwa likiendeshwa kwa kasi kabla ya kugonga watoto hao waliokuwa wamesimama kando ya barabara wakingoja kuvuka.

Monica Wanjiru ambaye alifanya mtihani wake wa kitaifa kwa Darasa la Nane katika Shule ya Msingi ya Sunrise Academy, Sachangwan, alipata alama 284 na alikuwa akitarajia kujiunga na shule ya sekondari Januari.

Babake, Michael Njoroge alijutia kisa hicho na kuongeza kilikuwa kisa cha pili kwa mtoto kuaga dunia mahali hapo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.