Askofu kuenda kortini baada ya upatanisho kugonga mwamba

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Ndung’u Gachane

UONGOZI wa kanisa la AIPCA unaelekea mahakamani baada ya mazungumzo yaliyoongozwa na Ikulu kugonga mwamba kwa mara ya tatu.

Kulingana na askofu ambaye anaongoza sehemu moja ya kanisa hilo, mazungumzo hayakufanyika baada ya baadhi ya viongozi kukataa kufika.

Askofu Julius Njoroge alisema mazungumzo hayo yamefanywa kwa miezi sita ila hakujakuwa na suluhu, na kushutumu wapinzani wake kwa kuchelewesha mazungumzo hayo.

Ikulu imekuwa ikiongoza majadiliano miongoni mwa maaskofu watatu wa AIPCA - Julius Njoroge, Samson Muthuri na Fredrick Wang’ombe ambao wamekuwa wakizozania uongozi wa kanisa hilo kwa miaka miwili.

Kulingana na Askofu Njoroge, Ikulu iliwateua maaskofu waliostaafu Lewis Emathew na Peter Njenga kutoka Kanisa la Methodist na Anglican mtawalia, na msimamizi wa fedha wa Ikulu ambaye aliteuliwa na Rais Uhuru Kenyatta kuongoza mazungumzo hayo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.